Habari

Vita vyaanza Ukraine, Rais Putin awataka waweke silaha chini, atoa onyo kwa atakayeingilia

Katika hotuba ya televisheni saa 05:55 saa za Moscow (02:55 GMT), Vladimir Putin wa Urusi alitangaza “operesheni ya kijeshi” katika eneo la Donbas mashariki mwa Ukraine. Putin alisema Urusi ilikuwa ikijilinda.

Aliwataka wanajeshi wa Ukraine kuweka chini silaha zao.

Uingiliaji wowote wa mataifa ya nje dhidi ya Urusi kutapata jibu la “papo hapo”, alisema

Urusi imeshambulia miundombinu ya Ukraine kwa makombora, Ukraine inasema. Pia inasema imedungua ndege za Urusi – jambo ambalo Moscow inakanusha.

Misafara ya wanajeshi na vifaru imeingia Ukraine kutoka pande zote. Msafara mmoja umevuka kutoka Belarus kuelekea kaskazini mwa mji mkuu wa Kyiv. Mwingine umeingia kutoka Crimea kusini, ambayo Urusi ilitwaa kutoka Ukraine mnamo 2014

Takriban watu wanane wanaripotiwa kuuawa

Lakini katika hatua yake hiyo ya kushtusha pia ameyataka majeshi ya Ukraine kuweka chini mtutu wa bunduki na kutoa onyo kwa yeyote atakaeingilia. Hatua hiyo ni baada ya wenye kutaka kujitenga kuomba msaada wa kijeshi kutoka katika serikali ya Urusi, jambo ambalo awali Umoja wa Ulaya uliita kama ya kuvuka uhuru wa kimipaka.

Kuna foleni ndefu za magari huku wakazi wakijaribu kuukimbia mji mkuu wa Kyiv. Wakaazi wengine wametafuta makazi katika vituo vya treni. Waandishi wa BBC wanasema ingawa watu walitarajia shambulio hilo, ukubwa wa uvamizi huo umewashangaza

Ukraine imetangaza sheria ya kijeshi. Waziri wa mambo ya nje Dmytro Kuleba amehimiza vikwazo vikali, ikiwa ni pamoja na kuipiga marufuku Urusi kutoka kwa mfumo wa kimataifa wa uhamishaji pesa.

Bei ya mafuta imepanda hadi zaidi ya $100 kwa pipa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka saba. Sarafu ya Kirusi, imeshuka hadi chini kabisa dhidi ya dola na euro. Masoko ya Uingereza yameshuka

Kumekuwa na matukio yakushutumu kutoka kwa viongozi wa dunia: Rais wa Marekani Joe Biden amesema vita hivyo vitaleta “kupoteza maisha kwa kiasi kikubwa. “Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema “amechukizwa”na “shambulio hilo lisilo na msingi wowote”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents