Vital’O: Yanga tunawaogopa hata tu
Uongozi wa time ya Vital’O ya Burundi umewataja wachezaji wa Yanga SC kipa Djigui Diarra na Viungo Max Nzengeli na Stephane Aziz Ki kama Kizingiti kwao kuwatoa Yanga SC katika Mashindano ya CAF.
Uongozi huo umesema wachezaji hao ni msaada mkubwa kwa kikosi hicho na kueleza kuwa mchezo wao wa klabu Bingwa Jumamosi utakuwa mgumu kutokana na nyota hao.
Akizungumza na Manara TV baada ya kuwasili nchini Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa timu hiyo Arsene Bucuti alisema nyota hao ni moto lakini watapambana.
“Kwanza tunamhofia Diarra ni kipa mgumu kufungwa kwa hapa Tanzania hata kama wanamfunga AFCON wengine ni Maxi Nzengeli, Aziz Ki, Pacome Zouzoua ni wachezaji pofessional ni wachezaji ambao wanajua wanachokifanya”.
“Zamani mashabiki wa Tanzania walikuwa wanapenda Vital’O kuliko Simba na Yanga kwahiyo tunao mashabiki wa kutosha hapa Tanzania. Tumewahi kuwapiga bao 7-0 sasa tunaaka kurudia tulichokifanya zamani alisema Arsene.
Timu hizo zitacheza pambano lake Jumamosi katika Uwanja wa Azam Complex Chamanzi nee kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.