Habari

Vitongoji nane wagombea wake walifariki dunia uchaguzi kurudiwa

 

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa amesema katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimepata ushindi wa jumla wa wenyeviti wa serikali za vijiji kwa nafasi ya viti 12,150 sawa na asilimia 99.01 huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikipata jumla ya viti 97 sawa na asilimia 0.79.

Huku akimesema Vitongoji nane wagombea wake walifariki dunia uchaguzi utarudiwa ambapo 37 havikufanya uchaguzi tarehe 27 Novemba, 2024. Kati ya hivyo, vitongoji havikufanya uchaguzi kwa kuwa wagombea wake walifariki baada ya zoezi la uteuzi. Wagombea hao walitoka katika Halmashauri za wilaya za Kilwa (2), Nanyumbu (1), Itilima (1), Ikungi (1), Manyoni (1), Uyui (1) na Mbarali (1),”amesema Mchengerwa.

Mchengerwa amesema hayo Novemba 28, 2024 wakati akitoa matokeo ya jumla ya uchaguzi huo.

Ambapo amesema vitongoji 29 havikufanya uchaguzi kutokana na sababu mbalimbali. Vitongoji 12 vitarudia uchaguzi kwa kuwa matokeo ya wagombea yalifungana. Vilevile, vitongoji 9 vitarudia chaguzi kutokana na wagombea pekee kutopata kura za kutosheleza

“Chama cha ACT kimepata viti 11 sawa na asilimia 0.09, Chama cha CUF kimepata jumla ya viti 10 sawa na asilimia 0.08, NCCR Mageuzi imepata kiti kimoja sawa na asilimia 0.01” ameongeza Mchengerwa.

Mchengerwa amesema katika nafasi za Mwenyekiti wa Kitongoji CCM imeshinda nafasi 62,728 sawa na asilimia 98.26, CHADEMA imeshinda nafasi 853 sawa na asilimia 1.34.

ACT Wazalendo imeshinda nafasi 150 sawa na asilimia 0.23,CUF imeshinda nafasi 78 sawa na asilimia 0.12, NCCR -Mageuzi imeshinda nafasi 10 sawa na asilimia 0.02, UDP imeshinda nafasi 6 sawa na asilimia 0.01, UMD imeshinda nafasi 2 sawa na asilimia 0.003 na ADC imeshinda nafasi 1 sawa na asilimia 0.002.

Vilevile Mchengerwa CCM kimeshinda viti 4213 sawa na asilimia 98.83 kwenye nafasi za Mwenyekiti wa Mtaa huku CHADEMA imeshinda nafasi 36 sawa na asilimia 0.84.

ACT Wazalendo imeshinda nafasi 9 sawa na asilimia 0.21, CUF imeshinda nafasi 4 sawa na asilimia 0.09 na CHAUMA imeshinda nafasi 1 sawa na asilimia 0.02.

Aidha, amesema katika mtaa mmoja wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga hakupatikana mshindi kwa sababu kura za wagombea wawili zilifungana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents