Habari

Vodacom M-Pesa yazindua huduma ya malipo ya Kimataifa popote ulimwenguni!

Vodacom Tanzania, kampuni inayoongoza katika hudumaza mawasiliano nchini, imezindua rasmi huduma yamalipo ya kimataifa (M-Pesa Global Payments), hatuainayoleta mapinduzi katika biashara na urahisi wa malipokwa wateja na wafanyabiashara wa Tanzania wanaosafirina kufanya biashara nje ya mipaka ya nchi, Pia kuongezaujumuishwaji wa kifedha kidigitali.

Kupitia ushirikiano na VISA, Alipay, Network International, Magnati na MTN Uganda, wateja sasawanaweza kufanya  malipo kwa kutumia mfumo wa Tap & Pay duniani kote kwa kugusisha simu yenye M-Pesa Visa card kwenye mashine ya malipo, kulipawafanyabiashara nchini China kupitia Alipay kwa mfumounaowezeshwa na Thunes, kufanya miamala Dubai kwawafanyabiashara waliounganishwa kwenye mfumo waTerraPay, pamoja na kuwalipa wafanyabiashara nchiniUganda moja kwa moja kwenye waleti zao za MTN MoMo., yote haya kupitia M-Pesa Super App au Menyuya M-Pesa.

Huduma hizi ni salama, rahisi kutumia na zinaondoachangamoto zinazotokana na mifumo ya kibenki. Kwapamoja, huduma hizi zimeifanya M-Pesa kuwa moja yamifumo ya malipo ya kidigitali iliyoendelea zaidi barani Afrika. Uzinduzi huu unawawezesha wateja wa Tanzania na wasafiri wanaofanya malipo ya mara kwa mara katikauwanda wa Afrika Mashariki, Mashariki ya Kati, Asia namaeneo mengine duniani, lakini hukabiliana na gharama, ucheleweshwaji au ukosefu wa usalama kwa baadhi yamifumo ya malipo.

Epimack Mbeteni, Mkurugenzi wa M-Pesa Vodacom Tanzania, alisema: “Ushirikiano wetu na VISA, Alipay, Network International na MTN Uganda unaonyeshadhamira yetu ya kujenga mifumo imara ya malipo yakidigitali. Kwa pamoja, tunawawezesha watu kufanyamalipo hata wavukapo mipaka ya Tanzania kwa urahisiule ule wanaoufanya ndani ya nchi, kwa usalama, harakana kwa gharama nafuu,” alisema Mbeteni. Mkurugenzihuyo aliongeza kwamba, “hili ndilo lengo kuu la M-Pesa: kuendeleza ujumuishwaji wa kifedha na kuhakikishaubunifu wa kidigitali unaowanufaisha wajasiriamaliwadogo, wa kati, wakubwa pamoja na wateja wenyemahitaji binfsi ya malipo. Kupitia nguvu hii ya pamoja, tunafungua njia mpya za biashara, kupunguza gharama za uendeshaji na kuwapa wateja uhuru mpana wa kushirikikatika uchumi wa kidigitali.”

Uzinduzi huu unaleta ubunifu mpya uitwao M-Pesa Tap & Pay kwa ushirikiano na Visa, ubunifu wa kwanza barani Afrika, unaowawezesha wateja kulipa duniani kotekwa kugusa tu simu zao zenye M-Pesa Visa card kwenyemachine za watoa huduma zenye mfumo wa Visa. Victor Makere, Meneja wa Nchi wa Visa Tanzania, alisema: “Kupitia ushirikiano huu, tunawawezesha mamilioni yawateja wa M-Pesa kufurahia malipo ya kidigitali yaliyosalama na rahisi popote Visa inapokubalika. Teknolojiaya Tap & Pay ni huduma inayomruhusu mteja kulipa kwakugusisha simu yake karibu na mashine ya malipo yenyemfumo wa Visa, bila kuingiza namba ya kadi au PIN. Malipo yanakatwa moja kwa moja kupitia M-Pesa Visa card iliyopo ndani ya simu kidigitali. Hii inaongezausalama na urahisi, ikiruhusu wateja kufanya malipoduniani kote bila kufichua taarifa zao nyeti. Ubunifu huuunaunga mkono safari ya Tanzania kuelekea uchumi wamalipo ya kidigitali na kuwawezesha wateja na biasharakulipa kwa njia za kisasa zaidi.”

Kupitia Mtandao wa Thunes, wateja wa M-Pesa sasawanaweza kulipa wafanyabiashara nchini China ndaniwanaotumia mfumo wa Alipay kwa kasi na usalama.Andrew Stewart, Afisa Mkuu wa Mapato wa Thunes, alisema: “Urasimishaji wa malipo ya kuvuka mipaka kwanjia ya kidigitali ni hatua muhimu inayoongezaupatikanaji wa huduma na kusaidia dhamira yetu yakuwawezesha mabilioni ya watumiaji kushirikikikamilifu katika uchumi wa dunia. Kupitia ushirikianowetu na Vodacom, sasa tunawezesha biashara za Tanzania kuwalipa wafanyabiashara wa China papo hapokupitia mtandao wa Alipay. Kiwango hiki kipya cha uunganishaji na ubunifu kinaongeza imani katika mifumoya kifedha ya simu na kufungua fursa mpya za biasharaya kimataifa

TerraPay, ambayo inawezesha malipo ya kimataifa kwawafanyabiashara, inawaruhusu watumiaji wa M-Pesa kufanya miamala na wafanyabiashara waliopo Dubai kupitia mtandao wao mpana wa malipo. Willie Kanyeki,Makamu wa Rais wa TerraPay Kusini mwa Jangwa la Sahara, alisema: “TerraPay tunaamini katika uunganishajiwa mifumo na kuwezesha malipo bila mipaka. Ushirikiano wetu na Vodacom unapanua fursa za biasharakwa njia salama, kwa Watanzania wanaofanya shughuliDubai, na kuwaunganisha watumiaji wa Afrika namasoko mapya ya dunia.”

Kwa upande wa malipo kidigitali nchini Uganda kupitiaMTN MoMo, MTN ina mchango muhimu katikakurahisisha biashara za kikanda kwa wajasiriamaliwadogo na wa kati. Richard Yego, Mkurugenzi wa MTNMobile Money Uganda, alisema: “Ushirikiano huu nihatua muhimu kuelekea biashara huru na endelevu katikaukanda huu. Pamoja na Vodacom, tunafungua upatikanajimkubwa wa huduma za kifedha kwa maelfu yawafanyabiashara wanaovuka mipaka ya Uganda naTanzania, hasa wale wa sekta ya biashara ndogo na za kati ambao ndio uti wa mgongo wa uchumi wetu.”

Kwa kuzingatia matumizi makubwa ya huduma za fedhakwa simu na ongezeko la simujanja nchini Tanzania, masuluhisho haya ni nyenzo muhimu kwa wateja wakawaida pamoja na biashara ndogo na za kati zinazohitajihuduma za kifedha za uhakika, za haraka na rahisi.

M-Pesa ikiendelea kupanuka kama huduma salama narahisi ya malipo ya kimataifa, Vodacom Tanzania inaendelea kutekeleza dhamira yake ya kujenga uchumijumuishi wa kidigitali na kubadilisha maisha kupitiateknolojia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents