Habari

Vodacom Tanzania yakabidhiwa cheti cha usajili kwenye Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alizindua Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi pamoja na mifumo ya usajili na malalamiko ya ukiukwaji wa misingi ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi katika kituo cha Mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam tarehe 03 April 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan akimkabidhi cheti cha usajili wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi Mkurugenzi wa kitengo cha Sheria wa Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC Olaf Mumburi mara baada ya kuzindua tume hiyo jijini Dar es Salaam tarehe 3 April mwaka huu.

Tukio hili lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, mawaziri, mabalozi, pamoja na wageni mbalimbali.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom wakiwa katika eneo la hafla mara baada ya kukabidhiwa cheti cha usajili

Makampuni, mashirika, na taasisi mbalimbali zimetunukiwa cheti cha usajili kwenye Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi. Moja ya makampuni yaliyotunukiwa Cheti hicho ni Vodacom Tanzania. Hii ni baada ya kuwa kampuni ya mwanzo kusajili ulinzi wa taarifa binafsi za wateja wake hapa Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents