Vodacom Tanzania Yazindua Vituo vya Huduma za Matengenezo kwa Wateja Wake

Dar es Salaam – 25th September 2024: Vodacom Tanzania Plc imezindua vituo vya huduma za matengenezo kwa ushirikianona watengenezaji wa simu za Neon Ultra, Samsung, Vivo, Motorola, Honor na Oppo. Lengo la ushirikiano huu ni kutoahuduma bora kwa wateja ikiwemo kupata matengenezo ya simuzao katika maduka ya Vodacom katika maeneo mbalimbalinchini huku duka la Vodacom Mlimani City ikiwa kama mfanowa huduma hizo.
Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Philip Besiimire, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo naUsambazaji, George Lugata akisisitiza malengo ya kampunihiyo alisema, “Kipaumbele chetu daima ni kutoa huduma bora kwa wateja wetu na huduma hii mpya ni mwendelezo wake. Kwa kushirikiana na washirika wetu hawa, tunawezakuhakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma kirahisi nakwa ufanisi zaidi. Uzinduzi huu ni mwanzo tu, tunapangakuongeza vituo zaidi ili kukidhi mahitaji yanayozidi kuongezekakote nchini.“
Kwa sasa, Vodacom ina vituo 11 vya huduma za matengenezokatika sehemu kadhaa nchini. Hata hivyo, kutokana nakuongezeka kwa matumizi ya simu, kampuni hiyo inapangakupanua mtandao wa vituo vyake vya matengenezo ili kusaidiawateja wengi zaidi. Kwa kuanzia kampuni hiyo itafanyamatengenezo ya simu zilizotajwa huku ikiwa na mpango wakukaribisha makampuni mengine ya simu kuungana nao ilikuongeza ujumuishwaji wa kidijitali nchini.
Naye akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Huduma kwaWateja, Harriet Lwakatare, Meneja wa Maduka Rejareja, Vanessa Mlawi, alisisitiza umuhimu wa vituo hivyo, “hudumahizi za vituo vya matengenezo sio tu zinaongeza ujumuishi bilakubagua wateja bali pia zinaimarisha chapa ya kampuni yetu yaVodacom. Inatusaidia kushughulikia changamoto za wateja hukupia ikitoa fursa ya kuuza bidhaa na huduma zingine za Vodacom. Zaidi, vituo hivi vinatupa mwangaza kujua mahitaji ya watejawetu, na namna bora ya kuboresha huduma zetu.“
Mbali na kuboresha huduma kwa wateja, ushirikiano huuunaendana na dhamira ya Vodacom ya kuwa kinara wamabadiliko ya kidijitali kote nchini. Vituo vya matengenezovitasaidia kuwahudumia wateja wa kampuni hiyo huku pia vikiongeza matumizi ya simu na uelewa wa kidijitali.
Kama kampuni inayoongoza katika sekta ya mawasiliano nateknolojia nchini Tanzania, ikiwa na wateja zaidi ya milioni 22, Vodacom inaendelea kuongoza katika utoaji wa hudumazinazomjali mteja huku zikikidhi mahitaji yanayoongezeka yawatumiaji wake.
Pamoja na kuwa na mpango wa kuongeza vituo vyamatengenezo kwenye maeneo mengine, Vodacom inaendeleakujitolea kuhakikisha wateja wake wanapata huduma za matengenezo za kuaminika na hivyo kuridhika na huduma za kampuni hiyo.