Vodacom wafanya maboresho makubwa ya mtandao kuwahakikishia wateja wake huduma bora
Kampuni kinara yateknolojia na mawasiliano nchini, Vodacom Tanzania, imetangaza kufanya mabadiliko makubwa katika miundombinuya mtandao wake ikiwa ni sehemu ya kuwahakikishia watejawake huduma bora na za kisasa zaidi.
Akizungumzia hatua hii, Mkurugenzi Mtendaji wa kampunihiyo, Philip Besiimire alisema kuwa Vodacom imejidhatiti kuwakinara katika ubunifu na kuboresha huduma zake kila wakati. “Ili kuendelea kuwa kinara katika teknolojia na kuwapatiawateja wetu huduma bora, tumewekeza kwa kiwango kikubwakatika kuboresha miundombinu ya mtandao wetu,” alibainisha.
Hatua hii ni muhimu kwa kuwa inaiandaa nchi na wateja wetukuwa tayari kupokea mabadiliko ya teknolojia ya kisasa kamavile Akili Mnemba (AI) ambayo inalenga kuleta maboreshomakubwa ya upatikanaji wa huduma za mtandao kwa wateja.
Besiimire alifafanua kuwa maboresho haya yanalenga kuongezakasi, kuimarisha mtandao na kuhakikisha huduma zinaendeleakubaki imara ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka kila kukicha.Ingawa jitihada hizi ni hatua kubwa mbele, pia zinapitiamchakato mgumu ambao unaweza kuathiri upatikanaji wahuduma katika maeneo kadhaa kwa kiasi fulani.
“Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote ambao umewaathiriwateja wetu na tunawahakikishia kwamba tunafanya kilajitihada kupunguza usumbufu huo. Zoezi hili linatarajiwakukamilika ifikapo katikati ya Novemba, ambapo tutakuwa namtandao wenye nguvu na unaotegemewa zaidi kwa manufaa yawateja wetu wote,” alisema huku akiongeza kuwa timu yakeitaendelea kuufahamisha umma wakati wote wa zoezi hili nakutoa msaada wowote utakapohitajika.
Sambamba na maboresho haya, kumekuwa na upanuzi wamtandao kote nchini huku kampuni ikiimarisha mtandao wake. Mkurugenzi wa Mtandao wa Vodacom Tanzania, Andrew Lupembe, alisema kuwa Vodacom Tanzania inafanya uwekezajimkubwa ili kupanua na kuimarisha mtandao wake.
“Mpaka sasa tumetumia asilimia 96 ya bajeti iliyowekwa kwaajili ya miundombinu ya mtandao. Kwanza, tumetanua matumiziya mtandao wetu kupitia uwekezaji wa NICTBB na Africa One. Pia tumeongeza uwezo wa vituo vyetu vya mtandao nakufungua vituo vipya Tanzania Bara na Visiwani,” alisema.
Lupembe aliongeza kuwa uwekezaji huu pamoja na uhimarishajiwa mifumo ya kampuni, utaleta huduma bora zaidi nainayoaminika katika wiki zijazo. “Wateja wetu watawezakufurahia kasi zaidi, ulinzi ulioboreshwa wa mtandao, nahuduma bora za mtandao bila changamoto yoyote,” alihitimisha