Vodacom waungana na Bolt kukuza ujumuishwaji wa kifedha kidigitali
Vodacom Tanzania Plcimetangaza ushirikiano wa kimkakati na Bolt, moja kati yamakampuni makubwa ya teksi mtandao, wakitoa huduma za usafiri nchini, kwa lengo la kuongeza ujumuishwaji wa kifedhakwa madereva na kukuza malipo ya kidijitali. Ushirikiano huuutaleta huduma za miamala ya kifedha kidijitali kwa maderevawa Bolt, wakiwemo madereva wa Magari, Bajaj na Bodaboda, kupitia mfumo wa M-Pesa kutoka Vodacom.
Ushirikiano huu utatoa fursa za kipekee kama mfumo wa malipobila kutumia fedha taslimu wa ‘Lipa kwa Simu’, mikopo yasimu, aina mbalimbali za bima, mikopo ya wafanyabiashara namkopo wa mafuta wa Chomoka, iliyotengenezwa mahsusi ilikuwawezesha madereva wa Bolt kutumia fedha zao kiusalamana kwa faida. Huduma hizi zitawarahisishia madereva utaratibuwa malipo na pia kuwasaidia kupata huduma muhimu kama vile matengenezo ya magari, mafuta na bima za vyombo vya moto.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa M-Pesa Vodacom Tanzania, Epimack Mbeteni, alisema, “Ushirikianohuu unaleta mabadiliko makubwa kwa madereva na wateja pia. Kupitia Lipa kwa Simu, tunawawezesha madereva wa Bolt kutumia mfumo salama, rahisi, na usio wa malipo ya fedhataslimu ambao utawawezesha kuongeza kipato chao na kupatahuduma muhimu kama mikopo ya mafuta na bima za ainambalimbali. Hatua hii ni sehemu ya jitihada zetu za kujengamfumo thabiti wa malipo bila fedha taslimu na kukuzaujumuishwaji wa kifedha hapa nchini.”
Naye Meneja Mkuu wa Bolt, Dimmy Kanyankole, alibainishafaida za ushirikiano huu kwa madereva na wateja wa Bolt,“tunafurahi kushirikiana na Vodacom Tanzania Plc kwakuunganisha huduma za M-Pesa na huduma za usafiri wa Bolt. Ushirikiano huu utafanikisha mchakato wa malipo kuwa rahisizaidi kwa madereva wetu na wateja, huku pia tukitoa huduma za ziada za kifedha zinazosaidia kuinua Uchumi wa madereva. Tunaamini ushirikiano huu utaimarisha sana ustawi wamadereva wetu na kuboresha huduma kwa watumiaji wa Bolt nchini Tanzania.”
Kupitia ushirikiano huu, Vodacom Tanzania na Bolt wanakusudia kuongeza thamani na idadi ya miamala ya kidijitalihuku wakipanua wigo wa huduma za kifedha kwa madereva waBolt na jamii kwa ujumla. Kwa kutoa mikopo, bima nakurahisisha huduma za malipo, ushirikiano huu unaunga mkonouwezeshaji wa kidijitali na kiuchumi kwa Watanzania.