Habari

Vodacom yarahisisha upatikanaji wa bima wiki ya nenda kwa usalama Mwanza

Taasisi za umma nchini zimeshauriwa kushirikiana na taasisi binafsikatika jitihada za kuhakikisha teknolojia inatumikaipasavyo ili kupunguza ajali za magari nchini.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimishohayo jijini Mwanza, mgeni rasmi Waziri Mkuu waJamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh MajaliwaKassim Majaliwa amesema kwamba taasisi za umma zina nafasi kubwa ya kushirikiana na taasisi za binafsiambazo nyingi zimejikita katika teknolojiainayowezesha kuepusha ajali.

Shirikisheni sekta binafsi ili kupata ujuzi na kujifunzakutoka kwao, hii itawawezesha kuboresha mifumo na hivyo kulinda maisha ya wananchi wetu ambayo yamekuwa yakipotea kwa ajali,” alisema Mh Majaliwa.

 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa (kulia) akiipongeza Vodacom Tanzania baada ya kupata maelezo ya vifaa vya kudhibiti mwendo na ajali vinavyofungwa kwenye magari ya wafanyakazi kutoka kwa Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni (kushoto), alipotembelea banda la kampuni hiyo, wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani kwenye viwanja vya Furahisha jijini Mwanza. Wakifuatilia maelezo hayo, wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. Adam Malima, na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Camilius Wambura.

Mh Waziri Mkuu aliongea hayo baada ya kupita katikabanda la kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc na kujionea jinsi ambavyo mfumo wakufuatilia magari ya kampuni na hivyo kuepusha ajalimahali pa kazi kwa miaka zaidi ya 10.

Aliongeza kwamba ili kudhibiti ajali zinazopotezamaisha ya wananchi, taasisi zina jukumu kubwa la kutafuta namna bora ya kulinda miundombinu na pia kuepusha majeruhi, “kwa miaka mitatu iliyopita (2020 – 2022) ajali nchini zilikatisha maisha ya watu 1582 nakusababisha majeruhi 4372, hili halikubaliki kabisa natunatakiwa kulidhibiti,” aliongeza Mh Majaliwa.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimishohayo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Adam Malimaamebainisha kuwa ni wajibu wa kisheria kwa kilammiliki wa chombo cha moto kukatia bima chombochake sio tu kwasababu ili asikamatwe na askari wausalama wa barabarani bali kwa faida yake, wamilikiwengine barabarani, abiria, na watembea kwa miguu.

Nadhani ipo haja ya kutoa elimu ya kutosha juu yafaida za bima kwenye vyombo vyetu vya usafiri. Sheria ya bima kwenye vyombo vya moto haijawekwa kwadhumuni ili dereva asikamatwe na askari wa usalamawa barabarani, hapana. Bima ipo kwa ajili yakukulinda, kwanza wewe dereva pindi utakapopatwa namatatizo barabarani, lakini pia ipo kwa ajili yakuwalinda wamiliki wengine barabarani, abiria, Pamoja na watembea kwa miguu. Na ndiyo sababu zipo bima za viwango tofauti,” alisema Mh. Malima.

“Kwa kuliona hilo, ningependa kuwapongeza Vodacom Tanzania Plc ambao ni mojawapo ya wadau wakubwawa wiki hii ya usalama barabarani kwa miaka mingimpaka imefikia wakati hatuendi kuwaomba tenaudhamini, tunajua ni sehemu ya tukio hili. Wenyewewanatumia teknolojia yao ya mawasiliano kuwawabunifu kwa kuja bidhaa ambazo zinabadili hali yaMaisha ya Watanzania. Kwa sasa wametuleteaVODABIMA, baada ya kuona kuwa kuna changamotokadhaa za kuzifikia huduma za bima, wao wakaamuakuitumia fursa ya mtandao mpana wa wateja walionaokuwarahisishia kuifikia huduma ya bima kwenye simuzao za mkononi. Ninaamini kila mmoja wenu hapaanamiliki simu ya mkononi, hivyo sioni sababu yakutoanza kutumia huduma hii ambayo imekurahisishiakuendelea na shughuli zako kwa sababu itakuwezeshakukata bima popote pale ulipo bila kwenda ofisini,alimalizia Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama ambayokitaifa inafanyika jijini Mwanza kuanzia Machi 14-17 ikiwa na kauli mbiu inayosema, ‘Tanzania Bila AjaliInawezekana, Timiza Wajibu Wako’.

Katika jitihada za kueneza matumizi na upatikanaji wahuduma ya bima nchini, kampuni ya Vodacom Tanzania Plc imewahamasisha Watanzania kutumiaVODABIMA, huduma inayopatikana kwa urahisikupitia M-Pesa inayowawezesha kujiunga mahali namuda wowote walipo kwa kulipia kidogo kidogomwaka mzima.

Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni alisemakuwa VODA BIMA inayopatikana kupitia huduma yaM-Pesa imekuja kufanya mapinduzi makubwa kwakuondoa mlolongo kwa Watanzania ambaowanapatikana sehemu tofauti nchini kuzifikia hudumaza bima kwa urahisi, kulipia kidogo kidogo kwa mwakamzima, na kujulishwa kwa njia ya ujumbe mfupi wamaneno endapo inataka kuisha.

Kupitia VODA BIMA inayopatikana kwenye M-Pesaanaweza akajiunga huduma ya bima kwa ajili yachombo chake cha moto na kuanza kulipia kidogokidogo kwa mwaka mzima. Pia, mteja atakuwaanajulishwa kwa kutumiwa ujumbe mfupi wa manenokujua mustakabali wa bima yake kama inakaribiakuisha ili alipie. Kwa sasa huduma hii inapatikana kwawamiliki wa vyombo vyote vya moto kama vile magarimadogo na makubwa, bajaji, na pikipiki. Lengo kuu la huduma hii ni kuisaidia serikali kuhamasisha wamilikiwote wa vyombo vya moto wanakuwa na bima kwa njiarahisi, salama, na haraka popote na muda wowote kwakulipia kidogo kidogo, alimalizia Bw. Mbeteni

VODA BIMA inayopatikana kwenye M-Pesa nihuduma ya kibunifu ya kiteknolojia iliyozinduliwa kwamara ya kwanza Julai 2021 na Vodacom Tanzania Plc kuwawezesha Watanzania kupata huduma za bima kwagharama nafuu na urahisi kwa kujiunga kupitia simuzao za mkononi na kulipia pesa kidogo kidogo kwamwaka mzima.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents