Voice Of Eagle,Wawosa waja na kongamano Dodoma
Leo tunapenda kuwahabarisha watanzania wote kuwa Taasisi ya Voice Of Eagle Tanzania kwa kushirikiana na taasisi ya Watu Wote ni Sawa (WAWOSA) kupitia mpango wake wa maendeleo kwa mabinti, tumeandaa kongamano la BINTI MWENYE NDOTO litakalofanyika tarehe 21.09.2024 kwenye ukumbi wa mikutano uliopo New Dodoma Hotel Jijini Dodoma. Taasisi hizi mbili ambazo zinafanya kazi ya uelimishaji Vijana, wanawake, Makundi maalumu na Jamii kwa ujumla tumeandaa kongamano hili kwa lengo la kuwasilisha ujumbe wa kupinga ukatili , mauaji na unyanyapaa dhidi ya watu wenye ualbino na tunatarajia kuwa na Mgeni rasmi ambaye Naibu waziri mwenye dhamana Mhe. Patrobasi Katambi (Mb)- Naibu Waziri , Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu. Pamoja na yote tutatumia jukwaa hili kutoa elimu mbalimbali za kibiashara, Teknolojia, Uongozi kwa mabinti wote ambapo watapata nafasi ya kukutana na wadau mbalimbali ambao wamebeba fursa za kimaendeleo kutoka serikalini na taasisi binafsi. Tunawakaribisha wadau mbalimbali kuwezesha kongamano hili na tutumie nafasi hii kuwaaalika mabinti wote kutoka Dodoma na Tanzania yote kushiriki kwenye kongamano hili ambalo washiriki wote hawatalipia mchango wowote na watalazimika kujisajili kabla, |
Baada ya kusema hayo niwashukuru wanahabari wote na niwatakie majukumu mema ya kuendelea kulihabarisha Taifa juu ya Mambo makubwa yanayofanywa na vijana wa Taifa hili.