Habari

Vyombo vya habari DW na VOA vyafungiwa Uturuki

Mamlaka ya Mashirika ya Utangazaji nchini Uturuki RTÜK imezifungia tovuti za shirika la utangazaji la Ujerumani Deutsche Welle na redio ya kimataifa ya Sauti ya Amerika VOA.

Mwenyekiti wa mamlaka hiyo Ilhan Tasci kuandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter usiku wa kuamkia leo kwamba tovuti za mashirika hayo yote mawili zimefungwa kufuatia amri ya mahakama iliyotokana na ombi la mamlaka hiyo ya Uturuki.

Tasci amesema mashirika yote mawili yalikuwa hayajawasilisha maombi ya vibali vya kufanyia kazi nchini humo. DW imethibitisha kwamba tovuti zake zote za lugha 32 zilikuwa hazifanyi kazi kunzia usiku wa jana nchini Uturuki huku VOA nayo ikithibitisha kufungiwa kwa tovuti yake.

DW na mashirika mengine ya habari ya kimataifa nchini Uturuki yamekuwa yakipokea vitisho tangu Februari, wakati ambapo shirika hilo linalosimamia vyombo vya habari Uturuki lilipoyataka mashirika hayo kuwasilisha maombi ya leseni kwa huduma zake zinazohitajika sana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents