Habari

Vyombo vya habari maarufu vyaitaka Marekani kuacha kumshtaki Assange

Vyombo vya habari maarufu vya Marekani na Ulaya vimeitaka Marekani kuachana na mashitaka dhidi ya muasisi wa mtandao wa Wikileaks, Julian Assange, vikielezea wasiwasi juu ya uhuru wa habari.

Katika barua ya wazi iliyoandikwa na magazeti ya the Guardian, the New York Times, Le Monde, Der Spiegel na El Pais, vyombo hivyo vimesema kesi hiyo dhidi ya Assange itaweka mfano mbaya, na inakwenda kinyume na kinachojulikana nchini Marekani kama ”Marekebisho ya kwanza ya Katiba” yanayohakikisha uhuru wa vyombo vya habari na kutoa maoni.

Assange aliyeko jela nchini Uingereza anatafutwa na Marekani, ili afunguliwe mashitaka 18 yanayohusiana na ujasusi na kuvujisha siri za jeshi la Marekani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents