Waalgeria waomba kulitumia dimba la Mkapa kuwakabili Mamelodi Sundowns 

Timu ya CR Belouizdad ya Algeria imeomba kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchi Tanzania kuutumia Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar Es Salaa kama kiwanja chake cha nyumbani kwaajili ya mechi ya Ligi ya Mbingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Mechi hiyo ya hatua ya makundi itachezwa Februari 28 mwaka huu kuanzia saa 12 kamili za jioni.

CR Belouizdad iliwasilisha ombi hilo kwa TFF ikitaka kucheza mechi hiyo jijini Dar Es Salaam na Shirikisho hilo lenyedhamana na soka nchini limekubali ombi hilo la CR Belouizdad baada ya kushauriana na Serikali.

Related Articles

Back to top button
Close