Waamuzi wa mechi ya Simba na Yanga hawa hapa

Waamuzi watakaochezesha mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Simba vs Young Africans utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Mei 8, 2021.

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF limeanika majina ya waamuzi watakaosimamia sheria 17 za mchezo wa soka siku ya mchezo wa Watani wa Jadi Simba na Yanga siku ya Jumamosi hii inayokuja.

Simba SC itashuka katika Uwanja wa Mkapa akiwa ndiyo timu mwenyeji kumkaribisha mtani wake Yanga SC kwenye mchezo huo wa tarehe 8, 2021 ambao huwenda kuweka wazi mbabe ni nani baina ya timu hizo mbili tangu kubadilisha makocha wapya.

Waamuzi wa mchezo huo wa Mei 8, 2021 ni kama ifuatavyo kwa mujibu wa Shirikisho la soka TFF. Mwamuzi wa kati atakuwa Emmanuel Mwandembwa kutokea mkoani Arusha, mwamuzi msaidizi namba moja Frank Komba kutoka Dar es Salaam, mwamuzi msaidizi namba mbili Hamdani Saidi kutokea Mtwara na Mwamuzi wa akiba akiwa ni Ramadhani Kayoko kutokea Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button