Habari

Waandamana kupinga gharama za umeme Afrika Kusini

Watu wanne waliuawa Jumatatu wakati wa maandamano ya kupinga kupanda kwa gharama za umeme katika kitongoji kimoja nchini Afrika Kusini, maafisa wamesema.

Wakazi wenye hasira kutokana na gharama kubwa za huduma msingi walifunga barabara na walichoma matairi na jengo la manispaa katika kitongoji cha Thembisa kaskazini mashariki mwa mji wa kibiashara wa Johannesburg.

Maafisa wamesema watu wawili waliuawa katika ufyatuaji risasi unaodaiwa kufanywa na polisi baada ya maandamano kuanza asubuhi.

“Inadaiwa kwamba walipigwa risasi,” msemaji wa polisi katika manispaa hiyo Kelebogile Thepa ameiambia AFP.

Baadaye jioni, Thepa alisema miili miwili zaidi ilipatikana karibu na mlango wa jengo lililochomwa, na kufikisha idadi ya waliofariki kufikia wanne.

Source Voice oF America

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents