Habari

Waandamana kupinga sherai za Corona Ujerumani

Maelfu ya watu waliandamana jana nchini Ujerumani kupinga vizuizi vya kuzuia kuenea kwa virusi vya corona na chanjo za lazima huku makundi madogo yakifanya maandamano kinzani.

Over 70,000 attend German protests against COVID measures | News | DW |  18.01.2022

Polisi inasema zaidi ya watu 7,500 walijitokeza mjini Dusseldorf ijapokuwa ni watu 3,500 pekee waliotarajiwa.Watu wengine 2,300 waliandamana katika eneo la Regensburg huku maandamano kinzani yakijaribu kuyavunja maandamano hayo.

Waandamanaji watatu wa maandamano kinzani waliwekwa chini ya ulinzi huku mwengine akikamatwa kwa kuwatusi na kuwashambulia maafisa wa polisi.Katika jimbo la Stuttgart, waandamanaji walisimama nje ya jengo la shirika la utangazaji la umma Südwestrundfunk (SWR) kulikosoa kwa utangazaji wake kuhusu janga la corona.

Waandamanaji hao waliliita ”chombo cha habari za uongo” huku wakisema ”wao ndio watu.” Chama cha waandishi wa habari wa Ujerumani DJV kimeyakosoa maandamano hayo na kupinga shtuma kwamba SWR inaambiwa cha kuripoti.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents