HabariSiasa

Waandamana kupinga sheria kali ya Corona, China

Maandamano ya kupinga sheria kali za serikali ya China za kupambana na maambukizi ya UVIKO yameendelea katika miji kadhaa leo Jumatatu. Polisi wametumia nguvu kujaribu kuwaatawanya waandamanaji, na baadhi wamekamatwa.
Maelfu ya watu wameshuka mitaani kulalamikia masharti makali ya kuzuia kuenea kwa virusi vya uviko, chini ya sera ya serikali ya kiwango sufuri cha maambukizi ya ugonjwa huo. Maandamano sawa na hayo yalikuwa yakiendelea pia katika miji ya Beijing na Nanjing yakihusisha hasa wanafunzi wa vyuo vikuu.

Kujitokeza hadharani kupinga hatua za serikali ni tukio la nadra sana katika China inayotawaliwa na chama cha kikomunisti, lakini kulingana na mmoja wa waandamanji aliyejitambulisha kwa jina moja la Jiang, ugumu wa masharti waliyowekea umewatia ujasiri.

Chanzo ni jumba lililoungua moto mjini Urumqi

Kilichoanzisha maandamano haya ni hasira iliyotokana na vifo vya watu kumi waliouwa baada ya jengo lao kushikwa na moto katika mji wa Urumqi kenye jimbo la kaskazini magharibi la Xinjiang wiki iliyopita.

Taarifa zilizosambaa mitandaoni zilieleza kuwa juhudi za uokozi zilikwamishwa na masharti makali ya kutotoka nje katika kuzuia kusambaa kwa virusi vya UVIKO.

Zilisema huduma za wazima moto zilicheleweshwa, na baadhi ya watu waliogopa kulikimbia jengo hilo lililoungua kwa hofu ya kukiuka masharti ya vizuizi.

Maeneo mengi ya mkoa wa Xinjiang, ukiwemo mji wake mkuu, Urumqi, yamekuwa chini ya sheria hiyo kwa zaidi ya siku 100.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents