Habari

Waangalia Afcon huku upimaji wa afya ukiendelea

Junuari 2024 – Katika juhudi za pamoja, Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na mradi wa USAID Breakthrough ACTION imezindua monyesho ya kukutanisha wananchi kuangalia mechi za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) huku ikiwapatia huduma mbalimbali za afya kama chanjo, upimaji wa VVU na elimu ya afya kwa ujumla.

Kampeni hii ya kipekee, inayoratibiwa na shirika la Johns Hopkins Centre for Communication Program, kupitia mradi wa Breakthrough ACTION, unaofadhiliwa na USAID, ina lengo la kuchochea fursa kwa watanzania kuboresha afya zao kupitia kubadilisha mila na desturi hasi ili kuboresha afya.

Waislam nchini wametakiwa kuanzisha jukwaa la biashara ‘Muslims Commerce Chamber’ mwamvuli ambao utaongonisha waislamu kibiashara nchi nzima na kutoa mafunzo pamoja na kuwaongamisha masoko mapya ya biashara.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Taasisi ya Dhinurain Islamic, Sheikh Shamsi Elmi wakati akitoa mada katika Mkutano wa Wana taaluuma wa Kiislamu Tanzania ambapo umedai Waislamu wana hali mbaya kiuchimu na lengo la Mkutano huo ni kukomboa uchumi wa Waislamu Tanzania.

Amesema kuna wafanyabiashara wengi wanashindwa kupiga hatua kutokana na kukosa mafunzo na njia ambazo zitawawezesha kuwafikisha mbali katika biashara zao.

“Kama tunataka kuangalia uchumi wetu tuangilie uchumi wa wafanyabiashara wadogo wadogo, huku chini kuna watu wanakosa hata mlo mmoja wa siku, tukiwawezesha hawa au tukiwafikia tutakuwa tumeukomboa Umma wa Waislam,” alisema Elmi

Awali mwanazuoni huyo alibainisha jambo lingine ambayo linatakiwa kuangaliwa ili kufungua biashara kwa waislam ni kuwa na bodi ya halali ambayo itakuwa inatoa vibali vya biashara ambazo zimekidhi matakwa ya dini ya kiislamu.

Akitolea mfano amesema kunatakiwa kuwe na saloon za kiislam, mabucha pamoja huduma zingine ambazo zimethibitishwa na hiyo bodi kwani kuna waislamu wengi wanaogopa
kwenda kwenye huduma hizo kutokana na mazingira ambayo sio rafiki kwa dini ya Kiislam.

Naye Dr. Ali Said Sunkar ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislam Kenya amewataka vijana wawe na shauku ya kutaka kufanikiwa kutokana na fursa mbalimbali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents