Habari

Waasi wa RED-TABARA wauwa Wanajeshi katika shambulizi Burundi

Msemaji wa serikali ya Burundi amesema kwamba watu wenye silaha kutoka kundi la waasi la Red Tabara wameua watu 9 na kujeruhi wengine kwenye mashambulizi ya usiku kucha magharibi mwa mwa nchi karibu na mpaka wake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Red Tabara limekuwa likipigana na serikali ya Burundi kutoka kwenye vituo vyake ndani ya Congo tangu 2015. Kupitia ujumbe wa X iliojulikana kama Twitter, Red Tabara limesema kwamba limeshambulia vituo viwili vya kijeshi vya Burundi Jumapili usiku, wakati likiteka silaha pamoja na risasi, na kwamba wanajeshi 6 waliuwawa.

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye mwishoni mwa Desemba alisema kuwa Rwanda alikuwa ikitoa hifadhi pamoja na mafunzo kwa kundi hilo, kufuatia shambulizi lingine ambalo serikali yake ilisema lilikuwa takriban watu 20. Baadaye Burundi ilifunga mpaka wake na Rwanda, ambayo ilikanusha madai ya Ndayashimiye.

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

 

 

 

 

CHANZO: VOA SWAHILI

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents