
Wabunge wa Bulgaria jana Jumatano wamepiga kura ya kukosa imani na waziri mkuu wa taifa hilo Kiril Petkov.
Wabunge 123 walipiga kura ya kuunga mkono uamuzi huo dhidi ya 116 na kufanikiwa kuiondoa serikali iliyoingia madarakani miezi sita iliyopita.
Hatua hiyo sasa inafungua milango ya uchaguzi mpya lakini chama cha Petkov cha mlengo wa kati cha PP hakitakuwa na fursa ya pili ya kupendekeza serikali kwa bunge hilo. Kura hiyo inapigwa baada ya muungano unaotawala kupoteza wingi kufuatia mvutano juu ya matumizi ya bajeti.