HabariSiasa

Wabunge wawili wahukumiwa miezi sita jela Senegal

Mahakama moja nchini Senegal imewahukumu wanasiasa wawili kifungo cha miezi sita gerezani kwa kumshambulia mwenzao mjamzito.

Wanaume hao wawili walimpiga mbunge mwenzao wa kike wakati wa rabsha bungeni mnamo Desemba mosi. Massata Samb na Amadou Niang, ni wa kutoka chama cha upinzani cha PUR.

Waliamriwa kulipa jumla ya faranga milioni 5 kama fidia kwa mbunge huyo wa kike Amy Ndiaye. Ndiaye ni mbunge wa muungano tawala Benno Bokk Yakaar.

Akizungumza kwenye kesi hiyo, wakili wake alisema alilazwa hospitali baada ya tukio hilo na nusura ampoteze mtoto. Katika picha zilizoosheshwa kwenye televisheni ambazo ziliishtua Senegal, Samb alionekana akimzaba kofi Ndiaye baada ya kukejeli matamshi yake.

Alijibu kwa kumrushia kiti. Wabunge wengine kisha wakamsukuma Ndiaye sakafuni, kisha akapigwa mateke kwenye tumbo na mmoja wa watu waliohukumiwa jela.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents