Habari
Wachezaji Wafariki Dunia kwa ajali ya Boti

Takribani watu 25 wamekufa na wengine kadhaa kutoweka baada ya Mashua kupinduka katika Mto karibu na Mkoa wa Mai-Ndombe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti.
Miongoni mwa abiria wa Boti hiyo ni pamoja na wachezaji wa mpira wa miguu waliokuwa wakitokea kijiji cha Ngambomi baada ya kushiriki mechi.
Boti hiyo ilizama kilimota 12 baada ya kutoka bandari ya Mushie.
Kituo cha Polisi cha Mushie kilithibitisha kutokea kwa tukio hilo lakini hakikutoa taarifa zaidi.
Ajali za boti zimekuwa jambo la kawaida katika eneo hilo.Mwezi Disemba mwaka jana, boti iliyokuwa ikielekea katika mji wa Inongo ilizama karibu na mji wa Mai-Ndombe.