Habari

Wachimbaji wadogo wawili wa madini wahofiwa kupotea mgodini Mirerani

JESHI la Polisi mkoani Manyara, limesema watu wawili wanaosadikika kuwa wachimbaji wadogo maarufu wanaapolo  wanahofiwa kupotea katika machimbo ya madini ya Tanzanite, Mirerani.

Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi mkoani Manyara, Ahmed Makarani, amethibitisha huku akisema kutokana na kuwapo kwa taarifa nyingi ambazo hazina uhakika ameelekeza wasaidizi wake kufungua jalada la uchunguzi ili kupata ukweli wa jambo.

“Ni kweli tumefungua jalada la uchunguzi kufatilia hilo jambo, ili tuweze kupata vyanzo sahihi maana imekuwa na vyanzo vingi vipo vinavyosema wamepotea watu nane na vingine vinasema watu tisa,” amesema Makarani

Makarani amesema baada ya siku mbili watakuwa kwenye nafasi nzuri ya kujua ukweli ni upi kwa kuwa watakuwa wamepata wazazi ambao wamepotelewa na watoto wao na kuzungumza nao.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents