Bongo5 ExclusivesBurudaniHabari

Wadau na mashabiki wanalalamika wasanii, muziki umepoa

Kupitia kipindi cha RECAP NA MANDO @el_mando_tz amezungumzia namna game ya muziki wa Bogo Fleva ilivyopoa kwa sasa tofauti na miaka miwili mpaka mitatu iliyopita nyuma.

@el_mando_tz amemtolea mfano Diamond wakati yupo kwenye ubora wake ilikuwa haipiti siku bila kuwepo na tukio lolote ambalo litazungumziwa na kuufannya muziki wa Bongo Fleva kuwa midomoni mwa watu.

Ameongeza kuwa tunaweza tukachukulia poa namna matukio ambayo Diamond alikuwa anayatengeneza lakini kwa namna moja ama nyingine ndio yamesaidia kuutangaza zaidi muziki wetu kwa mataifa yanayaotuzunguka.

Haina haja ya kuyataja baadhi ya matukio ambayo Diamond alikuwa anayafanya kila mmoja anayajua matukio yake, kwa sasa Diamond ameamua kubadilika sana, ameamua kuwa CORPORATE maana ni Mkurugenzi wa media sasa na ndio maana hatengennezi Attention tena.

Kuna namna wadau na mashabiki wanatoa maoni yao kuwa game yetu kwa sasa imelala sana labda kidogo Harmonize anajitahidi lakini pia Marioo na Paula nao wanajitahidi.

Unahisi ni kwanini Game ya muziki wa Bongo Fleva imelala sana?? hakuna Attention tena??

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents