Wadau pamoja na Serikali wajikita kutatua changamoto zinazowakabili watoto wa Kike
KATIBU Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,Amon Mpanju amesema Serikali,kupitia wizara za kisekta kwa kushirikiana na wadau wamejikita kuhakikisha wanalenga kutatua changamoto zinazowakabili watoto wa kike nchini,ambazo zinatokana na kiwango kikubwa na mifarakano na migogoro kwa ngazi ya familia.
Ameyasema hayo Jana jijini Dar es Salaam wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya siku ya mtoto wakike duniani inayotarajia kufanyika wilayani Bahi Mkoani Dodoma,Oktoba 11,2024 alisema migogoro hiyo ya ngazi ya familia inapelekea kuwa na malezi duni na uangalizi hafifu kwa watoto hususan watoto wa kike.
Amesema kwa mujibu wa taarifa ya utafiti wa hali ya Afya ya uzazi na mtoto pamoja na viashiria vya maralia ya mwaka 2022 ilihainisha kwamba changamoto zinazowakabili watoto zimechangiwa kwa kiwango kikubwa na mifarakano na kutoelewana kwa ngazi ya familia na kupelekea malezi duni kwa watoto na kuwa katika uhatarishi huku wengine kuanza kufanya vitendo vya ngono mapema kabla ya umri halisi.
Mpanju amesema kwa mujibu wa taarifa hiyo inaonesha kwamba watoto wenye umri kati ya miaka 15 hadi 19 takribani asilimia 22 walipata mimba za utotoni ukilinganisha na asilimia 27 kwa mwaka 2015/16 utafiti wa namna hiyo ulipofanyika.
“Kwa mujibu wa utafiti huo ,inaonesha hali ya mimba vijijini kwa watoto ni asilimia 25 ukilinganisha na asilimia 16 kwa watoto wa mijini,watoto wetu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbali mbali ndani ya jamii ikiwemo vitendo vya ubakaji ,ulawiti na mimba na ndoa za utotoni,”amesema na kuongeza
“Kwa mujibu wa taarifa ya makosa ya ukatili wakijinsia na unyanyasaji ya Jeshi la Polisi kuanzia January hadi Disemba 2023 inaonesha matukio ya ukatili wa watoto yalikuwa 153001 ukilinganisha na matukio ya vitendo vya ukatili vya watoto kwa kipindi hicho kwa mwaka 2022 ambayo yalikuwa 12,163 na kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Jeshi la Polisi yenye matukio makubwa ya ukatili dhidi ya watoto mkoa wa kwanza Arshad, Morogoro,Tanga,Kinondoni pamoja na mjini maghharibi,”amesema Mpanju.