Wadau wa sanaa Tanga: Uchawi ulivyoathiriwa sanaa, Vijana wanakimbilia Dar wakiamini watatoboa (+Video)

Baadhi ya wadau mbalimbali wa Sanaa katika mkoa wa Tanga,wameeleza changamoto mbalimbali zinazopelekea sekta nzima ya sanaa kudidimia katika mkoa huo huku wakieleza vijana wengi wanakimbilia katika mkoa wa Dar Es Salaam wakiamini frursa ya kufanikiwa ipo katika mji huo.

Wakizungumza na Bongo5 tv pamoja na Bongo5.com mmoja ya mdamu alieleza kuwa yeye anahusika katika kusimamia mambo ya kisanaa hasa kusiamia wasanii ameeleza kuwa moja ya watru waliomfanya aingie katika suala la kusiamia wasanii ni kuona mafanikio ya baadhi ya wasanii wakiwemo Diamond Platnumz Alikiba Jux na wengine wakiyapata kupitia sanaa pia alitaja suala la uchawi kutawala katika masuala ya Sanaa kwa ujumla.

Hata hivyo walienda mbali zaidi na kuwaomba wawekezaji mbalimbali kujitokeza na kwenda mkoani humo kwa ajili ya kuwekeza katika Sanaa huku akiongeza kuwa sanaa hivi Sasa inafaida kubwa na katika mkoa wa Tanga Kuna vijana wenye vipaji lukuki akiwatolea mfano baadhi ya wasanii wanaotoka mkoani humo kama Roma Mkatoliki, Kassim Mganga na Mwana FA.

Written by  HASSANI .M.KAIMITE.

Related Articles

Back to top button