FahamuHabariTechnology

Wafahamu mabilionea 10 wakubwa zaidi duniani 2023

Kupitia jarida la World of Statistics limetoa orodha ya watu matajiri zaidi duniani au Mabilionea wa Wakati huu kulingana na Forbes, wameeleza kuwa Elon Musk ameondolewa namba moja kutokana na hasara aliyoipata mwaka 2022.
Jukwaa hilo la kufuatilia utajiri linatoa masahihisho yanayoendelea kuhusu thamani halisi na cheo cha kila mtu aliyethibitishwa na Forbes kuwa bilionea.
Hutokana na Thamani ya hisa za watu binafsi husahihishwa kila baada ya dakika 5 masoko ya hisa yanapofunguliwa tu.
Kwa mwaka huu 2023 hii ndio orodha ya watu 10 matajiri zaidi duniani, katika watu hao mabilionea 6 wanatoka Marekani.

1. Bernard Arnault: 

Ni mfanyabiashara mkubwa kutoka nchini Ufaransa, mwekezaji kwenye sekta za sanaa. Yeye ndiye mwanzilishi, mwenyekiti, na afisa mkuu mtendaji wa LVMH Moët Hennessy, Louis Vuitton, kampuni kubwa zaidi ya bidhaa za anasa (luxury) duniani. Utajiri wake unakadiriwa kuwa ni $190b

 2. Elon Musk: 

Ni mfanyabiashara mkubwa na mwekezaji mzaliwa wa Afrika Kusini kwa sasa akiishi nchini Maarekai, Yeye ndiye mwanzilishi, Mkurugenzi Mtendaji na mhandisi mkuu wa SpaceX; Mkurugenzi Mtendaji na mbunifu wa bidhaa wa Tesla, mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa Twitter, mwanzilishi wa The Boring Company; mwanzilishi mwenza wa Neuralink na OpenAI; na rais wa philanthropic Musk Foundation. Utajiri wake unakadiriwa kuwa ni $146b 

3.  Jeff Bezos:

Huyu ni mjasiriamali wa Kimarekani, mmiliki wa baadhi ya vyombo vya habari, mwekezaji, na mwanaanga wa kibiashara. Yeye ndiye mwanzilishi, mwenyekiti mtendaji, na rais wa zamani na Mkurugenzi Mtendaji wa Amazon.Utajiri wake uakadiriwa kuwa ni $120b

4. Gautam Adani:

Ni bilionea mfanyabiashara wa India ambaye ni mwenyekiti na mwanzilishi wa Adani Group, jumuiya ya kimataifa inayohusika katika maendeleo na uendeshaji wa bandari nchini India. Yeye pia ni rais wa Adani Foundation. Utajiri wake unakadiriwa kuwa ni $113b

5. Bill Gates:

Huyu ni mfanyabiashara mkubwa wa Marekani, mwandishi, mwekezaji, na mfadhili. Yeye ni mwanzilishi mwenza wa Microsoft. Utajiri wake unakaridiwa kuwa ni $111b

6. Warren Buffett:

Ni mfanyabiashara mkubwa wa Marekani, mwekezaji, na mfadhili. Kwa sasa ni mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Berkshire Hathaway. Yeye ni mmoja wa wawekezaji waliofanikiwa zaidi ulimwenguni na ana utajiri wa zaidi ya dola bilioni 110 kufikia Januari 2023, na kumfanya kuwa mtu tajiri zaidi wa sita ulimwenguni.

7.  Larry Ellison:

Ni mfanyabiashara na mwekezaji wa Marekani ambaye ni mwanzilishi mwenza na mwenyekiti mtendaji pia afisa mkuu wa teknolojia na afisa mkuu mtendaji wa zamani wa kampuni ya teknolojia ya kompyuta ya Marekani ya Oracle Corporation.Utajiri wake unakadiriwa kuwa ni $100b

8. Larry Page:

Ni mfanyabiashara mkubwa wa Marekani, mwanasayansi wa kompyuta na mjasiriamali wa mtandaoni pia anajulikana sana kwa kuanzisha Google na Sergey Brin. Utajiri wake unakadiriwa kuwa ni $89b

9. Steve Ballmer:

Ni mfanyabiashara na mwekezaji wa Marekani ambaye aliwahi kuwa afisa mkuu mtendaji wa Microsoft kutoka 2000 hadi 2014. Yeye ndiye mmiliki wa sasa wa Los Angeles Clippers ambayo inashiriki ligi Mpira wa Kikapu NBA.Utajiri wake unakadiriwa kuwa ni $86b

10. Carlos Slim:

Ni mfanyabiashara mkubwa wa Mexico, mwekezaji, na mfadhili. Kuanzia mwaka 2010 hadi 2013, Slim aliorodheshwa kama mtu tajiri zaidi ulimwenguni na jarida la biashara la Forbes. Alipata utajiri wake kutokana na umiliki wake mkubwa katika idadi kubwa ya makampuni ya Mexico kupitia kongamano lake, Grupo Carso.Utajiri wake unakadiriwa kuwa ni $85b

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents