Uncategorized

Wafanyabiashara wapigwa msasa, kuendesha biashara na kuweka kumbukumbu ya mapato

Benki ya Taifa ya Biashara leo imezindua kampeni yake ya Twende Sawa na NBC yenye lengo la kuwafuata na kuwapa elimu wafanyabiashara wanaochipukia katika maeneo yao ya kazi na biashara. Kampeni hiyo imezinduliwa leo katika hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali wakiwemo wafanyakazi na baadhi ya wateja wa benki hiyo.

Lengo kubwa la kampeni ya Twende Sawa na NBC ni kutoa elimu ya kuendesha biashara, usimamizi makini wa wapato, urasimishaji wa biashara pamoja na kuweka kumbukumbu za kifedha ili kumuwezesha mfanyabiashara anayechipukia kusimamia na kuendesha baishara yake kwa ufanisi zaidi. Pamoja na elimu itakayotolewa, kampeni ya Twende Sawa na NBC pia inatoa fursa kwa wafanyabiashara kufungua Akaunti ya Kua Nasi yenye masharti nafuu kufungua, inayotoa riba kwa amana za mteja pamoja na kutokuwa na gharama za uendeshaji za kila mwezi.

Akiongea katika hafla hiyo ya uzinduzi, Mkurugenzi wa Wateja wa Rejareja na Binafsi wa NBC, Nd Elibariki Masuke alisema kuwa lengo kubwa la Benki ya Taifa ya Biashara ni kuwa karibu zaidi na wafanyabiashara wadogo ili wawawezeshe kukuza  biashara sambamba na benki hiyo. Aidha alisema kuna maboresho ambayo benki hiyo imekuwa ikifanya ili kutimiza lengo la kuwa karibu zaidi na wafanyabiashara wadogo.

“Tumeongeza wigo wa matawi ya benki yetu nchini kupitia NBC Wakala na tumeweka mfumo wa kidijitali wa kufungua akaunti, tumerahisisha ufunguaji wa akaunti ambapo mtu anahitaji kitambulisho chake cha NIDA tu hivyo tumejipanga kuwaifikia na kuwahudumia kikamilifu wafanyabisahara wa jiji la Dar es Salaam na na maeneno mengine ya nchi kote.” Alisema Nd. Masuke.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents