Habari

Wafanyakazi wa ndani wanabakwa Saudi Arabia

Shirika la Amnesty International limesema Wafanyakazi wa nyumbani Raia wa Kenya walioko Saudi Arabia wanapitia hali za mateso ikiwa ni pamoja na kufungwa, ubaguzi wa rangi na mara nyingine kubakwa. Katika ripoti yao iliyotolewa leo Jumanne May 13,2025, Amnesty International imesema masharti ya kazi kwa Wakenya hao ni ya kikatili kiasi cha kufikia kiwango cha kile walichokiita kazi ya kulazimishwa na usafirishaji haramu.

Shirika hilo la kutetea haki za binadamu limeeleza kwa kina hali ya mateso wanayopitia zaidi ya Wanawake 70 waliokuwa wakifanya kazi za nyumbani nchini Saudi Arabia, Wafanyakazi hao wa ndani wanatajwa kupitia hali mbaya za maisha na unyanyasaji wa kibinadamu ikiwa ni pamoja na ukatili wa kingono, matusi na vipigo.

Amnesty International pia imesema Serikali ya Kenya inahusika moja kwa moja katika unyonyaji huo wa Wafanyakazi ambapo ripoti hiyo imetolewa wakati Rais wa Marekani Donald Trump akitarajiwa kufanya ziara rasmi leo mjini Riyadh.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents