Wafanyakazi waliopata ajira rasmi kunufaika

Tanzania leo imezindua rasmi kampeni mpya yaSalary Switch, inayolenga kuwazawadia Watanzania waliopokwenye ajira rasmi kwa zawadi za kila siku za pesa taslimu, mikopo ya mshahara ya kidigitali, na upatikanaji rahisi wamikopo hadi TZS milioni 150. Kampeni hiyo ya miezi mitatuitaanza tarehe 1 Mei hadi 30 Julai 2025, na inalengawafanyakazi wa sekta binafsi na ya umma, kuwapatia urahisi wakifedha wa haraka, motisha, na huduma bora za kidigitali.
Kupitia kampeni hii, wateja watakaohamishia mishahara yaoStanbic Bank wataweza kushiriki kwenye droo za bahati nasibuza kila siku (Jumatatu hadi Ijumaa), zenye zawadi za pesataslimu zinazotofautiana kati ya TZS 100,000 hadi TZS 500,000 kulingana na siku.
Zaidi ya hayo, wateja wanaofungua Akaunti ya Akiba ya Mtoto(Hatua) watazawadiwa na benki kwa kulinganisha kiasi cha awali kilichowekwa hadi TZS 250,000, ili kuwapa watoto waomwanzo mzuri wa kifedha. Kwa wateja waliofungua akauntihiyo tayari, kuweka amri ya kudumu ya kujiwekea akiba pia kutaleta zawadi kama hiyo – benki italinganisha kiasikinachowekwa hadi TZS 250,000.
Akizungumza wakati wa uzinduzi uliofanyika makao makuu yaStanbic Bank jijini Dar es Salaam, Emmanuel Mahondaga, Mkuu wa Kitengo cha Wateja binafsi na mauzo, alisema kuwakampeni hii inaonesha dhamira ya benki ya kuboresha hudumakwa wateja kwa suluhisho za kifedha bunifu.
“Tunatambua kuwa wafanyakazi na familia zao ni sehemumuhimu ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania. Kupitia zawadi za pesa kila siku, mikopo ya mshahara ya papo kwa papo hadi 60% ya mishahara yao, na fursa za mikopo hadi TZS milioni 150, tunahakikisha wateja wetu wanapata huduma za kifedhazinazowasaidia katika maisha yao ya kila siku,” alisemaMahondaga.
Priscus Kavishe, Meneja Mwandamizi wa Mauzo, alisisitizaumuhimu wa kuhamasisha utulivu wa kifedha na uwekaji waakiba kwa muda mrefu kupitia akaunti ya mtoto ya Hatua.
“Kupitia akaunti ya Hatua, tunawahamasisha wazazi kuwekezakwa ajili ya mustakabali wa kifedha wa watoto wao. Tutaendelea kulinganisha amri za kudumu hadi TZS 250,000 kwa mwezi wakati wa kampeni hii. Hii ni zaidi ya zawadi – nikuhusu kuwasaidia familia kujijengea uthabiti wa kifedha wabaadaye,” alisema Kavishe.
Kwa uwazi na usawa, kila mteja atakayefanikisha kuanzishaakaunti ya mshahara ya “Wezesha” atapokea ujumbe mfupi(SMS) kuthibitisha ushiriki wake katika droo ya kila siku. Washindi watatangazwa kila siku kuanzia mwezi wa pili wakampeni. Mchakato huu ni wazi na umeundwa ili kuwazawadiana kuwaunga mkono wateja wanaoichagua Stanbic kamamshirika wao wa kifedha.
Wateja wanaotaka kushiriki wanaweza kufungua akaunti zaokatika matawi yote ya Stanbic Bank au kwa kutumia programuya simu ya Stanbic au tovuti ya benki kwa urahisi na usalamawa kidigitali. Stanbic pia inashirikiana na waajiri kuhakikishamishahara ya wafanyakazi inahamishiwa moja kwa mojakwenye akaunti zao mpya.
Stanbic Bank Tanzania, sehemu ya Standard Bank Group – taasisi kubwa zaidi ya huduma za kifedha barani Afrika – inaendelea kutumia ubunifu kuwakwamua Watanzania nakuhakikisha huduma za kibenki zinapatikana kwa urahisi, usalama, na kwa manufaa zaidi.