Wafikishwa mahakamani kwa madai ya kuiba begi, simu venye thamani ya Sh. Milioni 1.9

Wakazi wawili wa Manzese Midizini mkoani Dar es salaam wamepandishwa kizimbani wakikabiliwa na mashtaka ya wizi wa begi na simu aina ya Samsung vyote vya pamoja vikiwa na thamani ya Sh.Milioni 1.9.
Washtakiwa hao ambao ni Khamis Ismail (25) na Fundi simu Jafari Ramadhan (33) wamefikishwa katika mahakama ya Mwanzo ya Kariakoo wakikabiliwa na mashtaka hiyo ya wizi wa begi na simu hiyo mali ya mlalamikaji Daniel Kimario.
Washtakiwa hao wamesomewa mashitaka yao na karani, Linda Kivaju mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo, Gladness Njau.
Akisoma mashtaka hayo, Kivaju amedai kuwa Julai 30, 2023 barabara ya Obama kata ya Kivukoni wilaya ya Ilala mkoani hapo washtakiwa wote waliiba begi lenye rangi jeusi lililokuwa na sh. 1,300,000 na simu moja aina ya Samsung yenye thamani ya sh. 630,000 vyote vikiwa na jumla ya sh. 1,930,000 mali ya mlalamikaji Kimario.
Amedai kuwa katika shtaka la pili Julai 30, 2023 huko Kariakoo kwa makusudi mshitakiwa simu aina ya Samsung yenye thamani ya sh 630,000 kutoka kwa Ismail kwa bei ya sh 30,000 huku akijua simu hiyo ni ya wizi.
Washtakiwa wote walikana kutenda makosa hayo na kupewa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wanaotambulika kisheria watakao saini bondi ya sh. laki tano kwa kila mmoja.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti 7, 2023 kwa ajili ya kutajwa.
Written by Janeth Jovin