Habari

Wafungwa zaidi ya 200 wametoroka gerezani Nigeria, Baada ya watu wenye silaha kuvamia

Maafisa katika jimbo la Nigeria la Kogi 240 wametoroka baada ya watu wenye silaha kuvamia gereza katika eneo la Kabba-Bunu. Mamlaka ya huduma za magereza nchini Nigeria inasema kuwa washambuliaji walikuwa wamejihami kwa silaha.

 

Kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa kuwa maafisa wawili wa usalama waliuawa wakati wa tukio hilo.

Taarifa zinasema wakati wavamizi walipofika, walikabiliana na walinzi wa gereza, na ndipo walipofanikiwa kuingia ndani ya gereza baada ya kuwazidi nguvu maafisa wa usalama wa ngereza hilo.

Maafisa bado hawajatoa taarifa kuhusu idadi ya watu waliouawa au majeruhi katika makabiliano hayo yaliyotokea Jumapili usiku.

Mamlaka ya huduma za magereza nchini Nigeria imesema kuwa kulikuwa na jumla ya wafungwa 294 katika gereza hilo wakati shambulio lilipotokea, 240 kati yao walikuwa wakisubiri kesi zao, na 70 walikuwa tayari wamehukumiwa.

Kamishna mkuu wa magereza Halliru Nababa tayari amekwishaagiza kukamwatwa wafungwa waliotoroka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents