AfyaHabari

Waganga wakuu, Famasia waaswa kufuata taratibu utoaji dawa 

Serikali imewataka Waganga Wakuu na Wafamasia katika Halmashauri nchini kufuata taratibu za utoaji dawa kwa wagonjwa ili kuepuka malalamiko yasiyokuwa ya lazima.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Dkt Festo Dugange leo tarehe 05.12.2022 alipokwenda kujionea utoaji wa huduma za afya kwa wananchi na maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Uhuru iliyopo Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma

“nataka mukikishe dawa zote muhimu zinapatikana kwa wagonjwa wote na zipatikane kwa asilimia 95 mpaka 100 sitarajii kupata malalamiko yoyote kwa wagonjwa ya kukosa dawa na wale watakaobainika na upotevu wa dawa hatua stahiki za kiutumishi zichukuliwe” alisema Mheshimiwa Dugange.

Mheshimiwa Dugange amesema ni lazima kila Mfamasia kukabidhi dawa zinazotoka Bohari Kuu ya dawa kwa kuthibitisha kwa maandishi kuwa amepokea na anayekabidhiwa andike jila lake na kusaini hali akibaki na nakala ya ushaidi juu ya mwenendo wa utumiaji dawa kwenye hospitali ili kuondoa malalamiko na ukosefu wa dawa.

Aidha amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI itapeleka gari la wagojwa katika hospitali ya Uhuru ili kuweza kuboresha zaidi huduma kwa wagojwa kwani miundo mbinu inayoendelea kujengwa ni dhamira ya Serikali kuendelea kuboresha ili kutoa huduma inayotarajiwa.

Kwa upende wake Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chamwino ametaja changamoto zinazo ikabili hospitali ya Uhuru upungufu wa majengo ya kutolea huduma kama wodi ya kulaza wagojwa wa upasuaji, wagonjwa wa dharura na ajali pamoja na jengo la kufulia na kutakasa vifaa na stoo

Ameishuku Serikali kwa kutoa vitanda 12, meza 12 pamoja na mashine ya mionzi pamoja na kupokea Mradi wa ujenzi wa jengo la kutengeneza hewa ya oksijeni

Related Articles

Back to top button