Habari

Wagonjwa 19,371 wafika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ndani ya miezi mitatu

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kipindi cha miezi mitatu ya Januari hadi Machi 2018 imeona jumla ya wagonjwa 19,371 wenye matatizo mbalimbali ya moyo kati ya hao wagonjwa wa nje ni 18,481 na waliolazwa ni 890.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka JKCI imeeleza wagonjwa 105 waliofanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua kati ya hao watu wazima 53 na watoto 52. Kati ya wagonjwa 105 waliofanyiwa upasuaji 66 walifanyiwa na madaktari wetu bingwa wa magonjwa ya moyo watoto wakiwa ni 35 na watu wazima 31.

Upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab ulifanyika kwa wagonjwa 231 kati ya hao watoto ni 20 na wakubwa 211. Kati ya wagonjwa 231 waliotibiwa wagonjwa watu wazima 211 walifanyiwa upasuaji na madaktari wetu wa ndani.

Kwa kipindi cha miezi mitatu jumla ya kambi za matibabu nane za matibabu zilifanyika kwa kushirikiana na washirika kutoka nchi za Ujerumani, Israel, Australia, Marekani, India na Falme za Kiarabu. Katika kambi hizo jumla ya wagonjwa 39 walifanyiwa upasuaji wa kufungua kifua kati ya hao watoto 17 na watu wazima 22.

Wagonjwa 72 walifanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua kati ya hao watoto 20 na watu wazima 52. Pia wamefanya upasuaji wa kuunganisha mishipa ya damu (AVF- Arterio Venous Fistula) kwa ajili ya kusafishia damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo (Hemodialysis) 36.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents