Habari

Wajasiriamali wapewa mbinu za mafanikio

MWENYEKITI wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Kata ya Kivule, Amos Hangaya amewapa mbinu nne wajasiriamali wa Kata hiyo za kuwawezesha kufanikiwa kiuchumi.

Hangaya ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kivule ameyafanya hayo leo Tawi la Fedha katika maadhinisho ya wiki ya Umoja wa Wanawake wa CCM .

“Mimi leo nitazungumzia ujasiriamali tu, ukitaka kufanikiwa kuna mambo lazima uyafanye na mengine uache kufanya,”amesema.

Alitaja mbinu nne ambazo ni kujifunza ambapo mjasiriamali lazima awe na uchu wa kujifunza pamoja na kuwasiliana na waliofaniwa.

Amesema mjasiriamali anatakiwa kuwa na maono bila maono hakuna mafanikio, anatakiwa kufanya mawasiliano bora na kutumia mitandao ili kupata fedha.

Amewaasa kuwa karibu na watu sahihi, kuacha uoga, kufanya tathmini ya Marafiki waliowazunguka kama wanafaa kwa maendeleo na kama hawafai kuwaacha lakini sio kuwachukia.

Amos alitaja mbinu ya nne kuwa mwadilifu kwa kufanya matendo sahihi na kama unatabia za kuongopa acha badala yake urudi katika mstari sahihi.

Mlezi wa Tawi la Fedha ambaye ni Diwani wa Viti Maalum Dar es Salaam, Magreth Cheka aliwapongeza kwa kazi wanazofanya katika Tawi hilo ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya wanachama UWT kutoka 55 na kufika 450 waliosajiliwa kwa njia ya kielektroniki.

Aliwaahidi kuwachangia Sh 100,000 kwa ajili ya changamoto walizosema za ofisi kutokamilika madirisha na marumaru.

Aliwataka kuendelea kuongeza wanachama pamoja na kuwakumbusha kuhamasishana kujitokeza kuniandikisha kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali ya Mtaa.
written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents