FahamuHabari

Wajue Wafungwa waliosusia kula chakula kwa muda mrefu zaidi duniani

Wafungwa waliosusia kula chakula kwa muda mrefu zaidi duniani

.

Mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye alirejeshwa gerezani baada ya kulazwa katika hospitali moja mjini Kampala kwa muda mfupi alipougua kutokana na hatua yake ya kususia kula chakula.

.

Hayo yalijiri baada ya familia ya Besigye kuibua wasiwasi kufuatia kupokea ujumbe kutoka idara ya magereza Uganda iikiitaka familia hiyo itume daktari binafsi wa Besigye.

Mara ya mwisho kwa Besigye kufika mahakamani, alionekana kudhoofika kiafya.

Lakini unajua kuwa kuna wafungwa wengine waliowahi kugoma kula chakula dunia. Je walifanikiwa kufanya hivyo kwa muda gani na kipi kilichowachochea?

Irom Sharmila – aligoma kula kwa miaka 16

.

Irom Sharmila alianza mgomo wake wa kususia kula mnamo mwaka 2000 kupinga sheria yenye utata katika jimbo la kaskazini-mashariki la Manipur, ambayo iliipa nguvu zaidi jeshi la India.

Sheria hiyo inaruhusu wanajeshi wa India ambao wamepelekwa katika maeneo ambayo serikali inayachukulia kuwa “yenye vurugu” kukamata watu bila vibali na hata kupiga risasi kukusudia kuua katika hali fulani.

Mnamo mwezi Novemba 10, 2000, raia 10 waliokuwa wamesimama kwenye kituo cha mabasi katika Jimbo la Sharmila la Manipur walidaiwa kupigwa risasi na kuuawa na wanajeshi wa India ambao walidai walikuwa wakiwarushia risasi.

Tukio hilo, lililopewa jina la “mauaji ya Malom” na raia waliokuwa na hasira, na kuwa chanzo cha Sharmila kuanza mgomo wa kutokula. Aliapa kuendeleza mgomo huo hadi sheria hiyo itakapofutwa.

Bi Sharmila alipoanza tu mgomo huo, alikamatwa na kuwa hospitalini kwa miaka 16, akizungukwa na walinzi wenye silaha na timu ya madaktari na wauguzi ambao walimlazimisha kula virutubishi vya kioevu na dawa kwa njia ya bomba, wakati mwingine hadi mara tatu kwa siku.

Wakati huo wote, Sharmila alipata uungwaji mkono mkubwa ulimwenguni na hata alishinda tuzo bora kutoka kwa Tume ya Kutetea Haki za Binadamu ya Asia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents