
Wakala wa Erling Haaland amethibitisha kuwa tayari wamepanga kumuondoa mshambuliaji huyo Manchester City, na hivyo kufungua mlango wa matumaini ya kuhamia Real Madrid.
Raia huyo wa Norway alitua Etihad kwa mkataba wa pauni milioni 51 msimu uliopita wa majira ya joto, na msimu wake wa kwanza umekuwa bora ndani ya miamba hiyo ya soka ya Premier League.
Haaland amefunga mabao 33 katika mechi 33 kwa kikosi cha Pep Guardiola, huku 27 kati ya hayo akifunga kwenye Ligi na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye magoli mengi kwa msimu mmoja ndani ya City.
Hata hivyo, wakati mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 akiendelea kuvunja rekodi akiwa na jezi ya City, hatua yake inayofuata inaonekana kuwa tayari imepangwa, huku wakala wake Rafaela Pimenta akithibitisha kuwa itakuwa ndoto kwa Haaland kusaini Real Madrid.
Rafaela Pimenta ambaye pia ni wakala Pogba alichukua nafasi ya wakala mkuu wa Haaland baada ya kifo cha Mino Raiola mwaka jana.