Burudani

Wakala waliomsaidia Diamond kununua Helicopter na Jet (Video)

" Ni kweli amenunua zote, helicopter nzuri ni Dollar Mil 2 mpaka dollar Mil. 4"

Bongo5 imefanya exclusive na kampuni ya @Viiiaviation ambayo inafanya huduma ya kukodisha holicopter ambapo wamefunguka kueleza jinsi walivyomsaidia Diamond kununua helicopter pamoja na private jet yake.

CEO wa kampuni hiyo Yusuph Kazi amesema wao wamesimamia manunuzi ya helicopter pamoja na ndege na kwa sasa kinachosubiriwa ni hatua za kuziruhusu vyombo hivyo kuja Tanzania.

Bosi huyo hakuweka wazi bei ya helicopter ila amedai helicopter nzuri ni kuanzia dollar Milioni 2 mpaka dollar Milioni 5.

Akiizungumzia helicopter hiyo alisema ni yakisasa, ina injini mbili, ina uwezo wa kutembea usiku na mchana.

Pia alisema ina uwezo wa kusafiri masafa marefu kwa kuwz ina uwezo mkubwa wakuhifadhi mafuta.

Written and edited by @yasiningitu

Related Articles

Back to top button