Wakamatwa 27 kwa wizi wa kwenye ajali

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu 27 kwa tuhuma za kuiba mifuko ya saruji baada ya ajali ya malori mawili eneo la Mbagala Mission jijini Dar es Salaam.

Kamanda Jumanne Murilo.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda Jumanne Muliro ikiwa ni baada ya wizi wa saruji kutokea kutokana na ajali ilyotokea Oktoba 4, huko Mbagala.

Kamanda Murilo amesisitiza, Jeshi litashughulika kikamilifu kwa mujibu wa sheria na watu wote wenye tabia ya kukimbilia kwenye matukio ya ajali na badala ya kuokoa watu na mali, wao wanageuka kuwa wahalifu au wezi.

“Mara baada ya tukio la ajali jeshi la Polisi lilifanya msako mkali kwenye nyumba jirani ilipotokea ajali, ambapo lilifanikiwa kuokoa mifuko zaidi ya 368 ya saruji pamoja na watuhumiwa 27, bajaji na pikipiki zilizokua zikitumika kufanya usafirishaji wa saruji hizo nazo zimekamatwa,” amesema.

Kamanda Murilo amesisitiza kila aliyehusika kwenye wizi wa Saruji katika eneo hilo la Mbagala watakamatwa mpaka mtu wa mwisho na kufikishwa mahakamani kusudi wawe mfano kwa watu wenye tabia hizo.

BY : Fatuma Muna

Related Articles

Back to top button