Wakazi aeleza sababu inayowaingiza wasanii kwenye utumiaji na uuzaji unga

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Wakazi, amesema huenda wasanii wa muziki wa Tanzania wanajiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya pamoja na kusafirisha kutokana na kugeza aina ya maisha fulani.
Akizungumza katika kipindi cha Mkasi TV kinachoruka kupitia EATV, Wakazi amedai licha ya tabia hiyo ya kugeza bado anafanya utafiti zaidi ili kujua zaidi.
“Bado hilo suala nalifanyia utafiti sio tu muziki bali entertainment na drugs,” alisema. “Kwa sababu watanzania wana tabia moja ya kugeza, mtanzania akisikia kitu fulani kimekiki nje kila mtu anakigeza. Sasa sisi watanzania tuna tabia ya kushobokea vitu labda hii ndio kitu kinasababisha issue za drug zikaja,” aliongeza.
“Halafu sio tu upande wa matumizi bado kuna hili suala nasikia kuna watu wengine wanajihusisha kwenye biashara yenyewe, sawa mtaani hali ni ngumu kwahiyo mtu kuingia huko siwezi kumshangaa sana. Kwahiyo hicho kitu nimejaribu kufanyia uchunguzi sipati jibu kwa sababu wengine wanasema wasanii wanakuwa na stress wanaamua kutumia madawa lakini kuna wengine hawajawahi kupata stress lakini wanatumia madawa halafu akishatumia madawa ndio anasema ngoja nikaimbe.”