Habari

Wakazi wa Saudi Arabia pekee ndiyo watakaofanya Hija mwaka huu

Maafisa nchini Saudi Arabia wamesema ni watu 60,000 tu watakaoruhusiwa kufanya Hija, kulingana na wavuti wa Haramain Sharifain, ambao unaripoti kutoka katika misikiti miwili mitakatifu.

Maafisa nchini Saudi Arabia wamesema ni watu 60,000 tu watakaoruhusiwa kufanya hija

Aidha taarifa hiyo inasema ni wakazi wa Saudi Arabia pekee watakaoruhusiwa kufanya Hija mwaka huu, wakiwemo wageni wanaoishi nchini humo.

Wavuti huo unasema kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kusambaa kwa aina mpya za virusi ya corona kote duniani.

Mwaka jana Saudi Arabia pia ilipiga maarufuku raia kutoka mataifa mengine kufanya ibada ya Hija nchini humo ili kudhibiti virusi vya corona.Mahujaji wakiwa msikiti wa Makka, Saudi Arabia

Watu takriban milioni mbili vinginevyo wangetembelea Maka na Madina msimu wa kiangazi kwa ajili ya Hija hiyo inayofanyika kila mwaka kulingana na imani ya kiislamu.

Kumekuwa na hofu kwamba Hija inaweza kufutwa kabisa. Kwa kawaida Hija ni moja ya vipindi muhimu katika kalenda ya dini ya Kiislamu.

Maafisa nchini humo wanasema hii ndio njia pekee itakayowezesha kufanya mipango ya kutokaribiana ambayo itawezesha watu wawe salama. Saudi Arabia imerekodi visa vya corona 161,005 na vifo vilivyotokana na ugonjwa huo ni 1,307.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents