HabariSiasa

Wakenya wakasirishwa na kauli ya Gavana wa Nairobi kuagiza miti Malaysia

Gavana wa kaunti ya Nairobi nchini Kenya amesema ananuia kuagiza michikichi kutoka Malaysia kama sehemu ya hatua ya kuufanya mji mkuu kuwa “mji wa kijani”.

Gavana Johnson Sakaja pia amesema ataanzisha mpango wa “kijani” na utahusisha vijana wasio na ajira katika upandaji miti.

Mpango wa mazingira ungewapa washiriki vijana Sh2,400 ($20; £17) kila wiki kwa ushirikiano na Kenya Forest Services.

Baadhi ya Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wamekosoa mipango ya Gavana Sakaja, wakihoji ni kwa nini Kenya haiwezi tu kupanda miti yake badala ya kuiagiza kutoka nchi hiyo ya kusini-mashariki mwa Asia.

“Kwa nini unaweza kufikiria kusafirisha michikichi kutoka Malaysia ilhali tuna maelfu yao kwenye ufuo wa Kenya? Binafsi ninaweza kutoa mimea 100 ya futi 1 ya michikichi kutoka kwa shamba langu bila malipo. alisema mtumiaji mmoja wa mtandao wa Twitter

Lakini gavana huyo amewapuuzilia mbali wanaomkosoa akisema miti hiyo ni mchango na serikali ya kaunti ya jiji haitakuwa ikiwalipia.

Bw Sakaja, ambaye yuko kwenye dhamira ya kufanya jiji hilo kuonekana zuri na la kijani kibichi zaidi, alikuwa amesema michikichi hiyo itapandwa kando ya barabara jijini ambako kuna majengo mengi ya serikali.

Related Articles

Back to top button