Wakurugenzi wa Facebook, Amazon, Apple na Google kuhojiwa na Congress, juu ya taarifa za uongo mitandaoni

Siku ya Jumatano inatarajiw akuwa Wakurugenzi Wakuu wa kampuni za Teknolojia Mark Zuckerberg (Facebook), Jeff Bezos (Amazon), Tim Cook (Apple) na Sundar Pichai (Alphabet-Google) wanatarajia kuhojiwa na Baraza la Wawakilishi (Congress) juu ya namna wanavyokabiliana na taarifa za uongo kutoka kwenye makampuni yao.

Imeelezwa kuwa mahojiano hayo yatafanyika kwa njia ya video kutokaana na janga la Corona linaloendelea kuikumbuka dunia kwa ujumla, na mahojiano hayo yatakuwa  mbele ya Watunga sheria ambapo tayari nyaraka takriban milioni 1.3 zimeshakusanywa kutoka kwa Kampuni hizo.

Baadhi ya watu wanatamani kusikia pia kuhusiana na usalama wa taarifa za watumiaji kwa sababu kampuni hizo zinamiliki taarifa nyingi za watumiaji na tayari kuna changamoto nyingi zinazoonesha kuwa taarifa za watumiaji zinatumia vibaya.

Imeongezwa kuwa mahojiano hayo yatatoa kielelezo cha jinsi kampuni hizo zinavyokabiliana na taarifa za uongo hasa kutoka kwa Mamlaka zinazowasimamia au kuwadhibiti na wako tayari kufanya au kutokufanya kitu gani kwa mujibu wa sheria katika kukabiliana na taarifa batili.

Related Articles

Back to top button