HabariTechnology

Wanaanga wa Marekani na Urusi kutumia chombo kimoja kwenda angani

Wanaanga wa Marekani na wa Urusi watapaa pamoja wakitumia chombo cha Urusi baadaye leo, ikiwa safari ya kwanza ya namna hiyo tangu vita vya Urusi na Ukraine.

Sergei Prokopyev na Dmitry Petelin wa Urusi pamoja na Frank Rubio wa Marekani wanatarajiwa kuanza safari ya kuelekea katika kituo cha kimataifa cha anga za mbali, wakitumia chombo cha Soyuz cha Urusi kutokea katika mtambo wa Urusi ulioko Baikonur nchini Kazakhstan.

Safari hiyo itakayoanza majira ya saa nane GMT itachukuwa muda wa saa tatu hadi kituo cha kimataifa cha anga za mbali, ISS.

Mwanaanga wa Marekani Frank Rubio amesema ushirikiano kati ya shirika la anga za mbali la Marekani, NASA na shirika la Urusi, Roscosmos umeendelea kuwa mzuri licha mivutano mikali baina ya serikali za Washington na Moscow.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents