Habari

Wanahabari wakumbushwa kuandika kwa weledi habari za chakula na lishe

MKURUGENZI wa Idara ya Elimu na Mafunzo ya Lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Dk. Esther Nkuba amewataka waandishi wa habari nchini kuandika na kutangaza kwa weledi habari zinazohusu masuala ya chakula na lishe ili kufikisha ujumbe stahiki kwa jamii pasipo kupotosha.

Dk. Nkuba alitoa rai hiyo hivi karibuni wakati akifungua semina ya siku moja kwa waandishi wa habari, watangazaji pamoja na waandaji wa vipindi mbalimbali, ambayo ililenga kuwajengea uwezo katika kuripoti kwa ufasaha taarifa kuhusu masuala ya chakula na lishe.

Amesema ni muhimu waandishi wa habari kutafuta taarifa sahihi za chakula na lishe hasa kutoka kwenye vyanzo, chombo ama taasisi husika ili kuhakikisha wanaandika kwa usahihi masuala ya sekta hiyo na kuondoa upotoshaji unaoleta taharuki katika jamii.

“Waandishi wa habari hapa nchini na duniani kwa ujumla mnamchango mkubwa katika kuhabarisha na kuelimisha jamii katika masuala mbalimbali ikiwemo yanayohusiana na lishe na kuchochea mabadiliko ya tabia za ulaji kwa jamii ya watanzania,” amesema Dk. Nkuba na kuongeza

“Tunayasema haya kwa sabbau wapo baadhi ya waandishi wanaotoa taarifa ambazo si sahihi zinazohusiana na masuala ya chakula na lishe na kisha kuleta taharuki kwenye jamii, ili kuondoa hayani muhimu kuzingatia chanzo chako sahihi cha kukupatia habari.” amesema

Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Mafunzo ya Lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Dk. Esther Nkuba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na taasisi hiyo. (Picha na Janeth Jovin)

Naye Ofisa Uhusiano na Mtafiti wa Lishe kutoka TFNC, Hamza Mwangomela amesema yapo mambo ambayo yanajitokeza hususan katika mahojiano hasa ya waandishi kumuhoji mtu ambaye si sahihi na baadae kupotosha maana ya suala husika analoulizwa.

“Tumekuwa tukiwaita hawa wanaopotosha katika vyombo mbalimbali vya habari, moja ya majibu yao wanakiri kukosa uelewa wa kutosha katika masuala haya ya lishe na chakula,” amesema

Hata hivyo amesema licha ya kuwahita wahusika hao pia uwaandikia barua vyombo husika kwa hatua zaidi ili kupata maelezo ya kutosha na wale wakaidi wanapeleka taarifa zao katika mamlaka zinazowadhibiti ikwemo, Mamlaka za Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Kwa upande wake Ofisa Lishe Mtafiti Mwandamizi kutoka TFNC, Maria Ngilisho, amesema utoaji sahihi wa taarifa zinazohusiana na masuala ya chakula na lishe kutaisaidia jamii kuelewa kwa kina njia sahihi wanazopaswa kuzifuata kzingatia ulaji unaofaha.

Ofisa Lishe Mtafiti Mwandamizi kutoka Taasisi  ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Maria Ngilisho, akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents