Habari

Wanajeshi wa Kenya wa wasili mji wa Goma

Kikosi cha wanajeshi wa Kenya jana kiliwasili katika mji wa Goma Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kama sehemu ya operesheni ya pamoja inayolenga kupambana na waasi katika eneo la mashariki.

Ndege mbili zilizowabeba wanajeshi takriban 100 wa Kenya ziliwasili katika uwanja wa ndege wa Goma jana na kulakiwa na viongozi wa eneo hilo.

Luteni Kanali Dennis Obiero wa Kenya aliwaambia waandishi wa habari kwamba dhamira yao ni kuendesha operesheni kali pamoja na vikosi vya Kongo, na kusaidia katika kuwapokonya silaha wanamgambo.

Viongozi wa jumuiya ya mataifa saba ya Afrika Mashariki, walikubaliana mwezi Aprili kuanzisha kikosi cha pamoja kusaidia kurejesha usalama katika taifa la Kongo lenye utajiri mkubwa wa madini.

Kenya itawatuma wanajeshi 900 kama sehemu ya jeshi hilo la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents