Michezo

Wanamichezo wanaoongoza kulipwa mkwanja mrefu zaidi duniani, Ronaldo nafasi ya tatu

Kwa kipindi kirefu cha mwaka uliopita 2020, wachezaji walio katika nafasi nzuri walitengwa, wakifanya kazi kwa mshahara wa kiwango cha chini, wakishiriki katika michezo tofauti mbele ya viwanja visivyo na mashabiki hali iliolenga kukabiliana na mlipuko wa virusi vya corona ambao umewanyima mabilioni ya dola wanariadha hao.

Lakini kwa wachezaji bora zaidi ya bora , mambo hayakuweza kuwa vizuri , ukiangazia swala la kifedha.

Wachezaji 10 wanaolipwa fedha nyingi zaidi duniani walipokea kitita cha $1.05 b kupitia mishahara yao katika kipindi cha miezi 12 iliopita, ikiwa ni zaidi ya asilimia 28 ya wale waliopokea fedha nyingi Zaidi 2018, ikiwa ni dirisha la miezi 12 ambalo bondia Floyd Mayweather alijipatia $285 million, zote akizipata katika pigano la maonesho la 2017 dhidi ya Conor McGregor.

1.Conor McGregor {$180m}

Mwaka huu , McGregor amewashangaza wengi kwa kufanikiwa kukusanya dola milioni 180 katika kipindi cha miezi 12 iliopita baada ya kutumia umaarufu wake katika mchezo wa UFC kufungua biashara mbali na kufanya mauzo. Kiasi kikubwa cha fedha hizo kinatoka katika mauzo ya hisa zake katika pombe ya Whiskey ambapo alijizolea $150 million. Ni mara ya kwanza kwa mwanamieleka huyo kuchukua nafasi ya kwanza na mara yake ya pili katika orodha ya wanariadha kumi bora duniani mwaka 2018 ambapo alikuwa katika nafasi ya kujipatia $99 katika pigano lake na Mayweather.

McGregor anataka kuwekeza pato lake zaidi akatika pombe . Amewasilisha wazo la kutaka kuinunua klabu ya Manchester United , timu yenye thamni ya juu zaidi katika ligi ya Premia.

2. Lionel Messi {$130m}

Lionel Messi

Mchezaji wa pili bora duniani baada ya McGregor ni mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi. Lionel Messi aliuweka ulimwengu wa soka katika ati ati mwaka uliopita alipojaribu kuondoka katika klabu ya Barcelona, suala lililoongezwa nguvu na kandarasi iliofichuliwa iliomuonesha akilipwa fedha nyingi na klabu hiyo zaidi ya vile watu walivyotarajia.

Mbali na mshahara wake anafadhiliwa na Adidas pamoja na kampuni ya kutengeneza nguo ya Ginny Hilfiger, dadake mwanamitindo Tommy Hilfiger.

Mwezi uliopita , Messi alituma jazi yake alioisaini kwa kampuni ya dawa nchini China Sinovac ili kusaidia kupata chanjo 50,000 kabla ya mchuano wa Copa America.

Subirini matukio mengine wakati kandarasi yake itakapokamilika mwezi Juni.

3, Christiano Ronaldo {$120m}

Christiano Ronaldo

Cristiano Ronaldo alikuwa mtu wa kwanza duniani kupata wafuasi milioni 500 duniani katika mtandao wa facebook, Instagram na Twitter mwezi Februari na kufuatilizia hilo mwezi mmoja baadaye kwa kumpita nyota wa zamani wa Brazil Pele kwa ufungaji wa mabao alipofikisha magoli 770 katika mashindano yote mbali na kufunga hat-trick katika mechi dhidi ya Cagliari .

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 ambaye kandarasi yake ya miaka minne ina thamani ya $64m kila mwaka na inakamilika 2022 , ana kandarasi ya ufadhili na kamapuni ya Nike na ndiye mmiliki wa biashara ya nguo ya CR7, hoteli na maeneo ya kufanyia mazoezi.

4. Dak Prescot {$107.5m}

Dak Prescot

Bonasi ya $66 milioni aliyowasili nayo pamoja na kandarasi ya miaka minne ilio na thamani ya $160m inamsukuma nyota wa Dallas Cowboys Dak Prescott katika klabu ya watu wenye thamani ya $ 100 milioni wakati anaporudi kutoka katika jeraha la kifundo cha mguu.

Siku za usoni zinang’aa kwa klabu hii yenye thamani ya juu zaidi .

Prescott pia hivi majuzi alitangaza uwekezaji katika wa maeneo manne ya mkahawa wa Walk-On’s.

5. LeBron James {$96.4m}

Lebron James

Katika nafasi ya tano ni nyota wa mchezo wa vikapu nchini Marekani LeBron James, ambaye rekodi yake katika mchezo huo wa NBA ulimfanya kuchukua ushindi wa nne mwezi Oktoba .

Kiwango chake cha mchezo hakipungui na badala yake kinaongezeka kila uchao. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 anaendelea kutawala uwanjani na sasa pia ameigiza filamu ya SpaceJam : Tayari ametia saini kandarasi mpya na kampuni ya PepsiCo baada ya kuachana na mshirika wake wa siku nyingi Coca-Cola.

Pia hivi majuzi alinunua hisa katika kundi la kampuni za michezo Fenway sports , ambayo inamiliki Klabu ya Boston Red Sox , Liverpool Fc na Roush Fenways Racing.

6.Neymar Jr. {$95m}

Neymar Jr

Wafuasi wa Neymar milioni 282 katika mtandao wa Facebook, Instagram na Twitter wanamfanya yeye kuwa mwanamichezo wa tatu maarufu katika mitandao ya kijamii , akiwa nyuma ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi ni hatua inayomfanya kuvutia wafadhili wengi.

Mwaka uliopita alitangaza kuvunja mkataba wake na Kampuni ya Nike Jordan na akafanikiwa kuwa balozi wa nembo ya kampuni ya Puma. Mwezi uliopita Epic Games ilizindua mchezo wa kanda ya video Gamer katika mchezo wake maarufu Fortnite na kuanzisha shindano la kutaka kushinda kiatu chake Mar Jr.

7.Roger Federer{$90m}

Rodger Federer

Huku akiwa nje katika kipindi kirefu cha mwaka uliopita na Jeraha la goti, mchezaji wa tenisi Roger Federer alijipatia pato la $90m kutoka kwa ufadhili wa kampuni kama vile Rolex , Credit Suisse na Uniqlo.

Hatahivyo pato kubwa la nyota huyo wa tenisi litatokana na hisa zake katika kampuni ya vifaa vya wanariadha ya On, ambayo inadaiwa kusubiri uzinduzi wa hisa mwaka 2021.

8.Lewis Hamilton${82m}

Lewis hamilton

Baada ya kushindana katika shindano la magari ya langalanga ya awamu ya sita ya Formula 1 championship katika misimu saba mwaka 2020, dereva wa Mercedes Lewis Hamilton ameorodheshwa miongoni mwa wanamichezo kumi bora kwa mara ya pili baada ya kuchukua nafasi ya kumi 2017 $46 million.

Ushindi wake wa mara 11 msimu uliopita ulimsaidia kujipatia bonasi pamoja na ufadhili kutoka kwa kampuni ya nguo ya Tommy Hilfiger, Monster Energy na Puma. Pia alizindua kundi lake katika msururu wa mashindano ya Extreme E series.

9. Tom Brady{$76m}

Tom Brady

Akiwa na umri wa miaka 43, Tomm Brady alikuwa ameingia katika mwaka wake muhimu wa kazi yake.

Mchezaji huyo wa Tampa Bay Bucaneers alijiongezea ufadhili na kampuni ya miwani ya Christopher Cloos na kampuni ya nguo ya Juggernaut fanatics huku akijikusanyia mapato ya juu kama msemaji wa mashindano hayo na kama mtangazaji wa matangazo ya biashara.

Alishinda taji la nane la SuperBowl . Brady ambaye tayari alikuwa ameingia katika biashara kupitia kampuni yake ya TB12 hivi majuzi alizindua kampuni ya utayarishaji wa wa filamu NFT.

10.Kevin Durant {$75m}

Kevin Durant

Kevin Durant, ambaye amejiunga na timu ya mpira wa vikapu ya Brooklyn Nets baada ya kukaa nje katika msimu wa 2019-20 kutokana na jeraha la nyonga amekuwa mfanyabishara mkubwa anayemiliki vyombo vya habari kupitia Bradroom na kampuni yake ya Thirty Five Ventures. Alikuwa mtayarishaji wa filamu ya Two Distant Strangers , ambyo ilijishindia tuzo ya filamu bora mwezi uliopita. Na alinunua hisa za klabu ya MLS Philadelphia Union mwisho wa msimu uliopita.

Durant pia alijipatia donge nono mwaka uliopita wakati kampuni ya Uber iliponunua Postmates, baada ya kuwekeza $1 million mwaka 2016 kwa bei iliopunguzwa.

Credit by BBC.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents