Habari

Wananchi wamuuwa aliyemshambulia Askari

Kijana anayekadiriwa kuwa na miaka 20-25 amefariki dunia kwa kushambuliwa na wananchi baada ya kumjeruhi kwenye taya na kidevu Askari wa Usalama Barabarani kwa kumpiga na chuma cha kupondea mawe (Moko), wakati akiwa kwenye eneo lake la kazi Mtaa wa Mwembeni, barabara ya Katoro Ushirombo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe, akionesha chuma kilichotumika kumjeruhi Askari

Kwa mujibu wa Eatv. Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kuvamiwa na kujeruhiwa askari wa barabarani namba H1619 John Charles lililopelekea wananchi wenye hasira kali kuingilia kati na kumuuwa muhusika kwa kipigo.

Aidha, Kamanda Mwaibambe amewataka wananchi wenye migogoro binafsi na Askari kuacha kujichukulia hatua mkononi badala yake watoe taarifa kituo cha polisi kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zinazostahiki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents