Wananchi wanawatishia mapanga mafundi mradi wa maji Bukoba (+ Video)

Mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawiro amepiga marufuku vitendo vya wananchi wa kijiji Rwagati kuwatishia kwa mapanga mafundi wanaotandaza mabomba katika mradi wa maji wa Kemondo-Kanazi wenye thamani ya shilingi bilioni 14.8 baada ya kuwatuhumu kukata migomba yao.

Kabla ya onyo hilo la Mkuu huyo wa wilaya, ni kuwa wananchi hao walikuwa wakiwatishia mafundi kuwakata kwa mapanga baada ya mafundi hao kufyeka migomba ya wananchi kwa ajili kuchimba mtalo wa kupitisha mabomba ya maji, nje ya eneo walilokubaliana awali kupitisha mabomba hayo ambalo pia mafundi hao walishafyeka migomba iliyokuwepo.

Bofya hapa kushuhudia.

 

https://www.instagram.com/tv/CP7lEXRhGNK/

 

Related Articles

Back to top button