AfyaHabari

Wananchi wenye makundi adimu watakiwa kuchangia damu

KUELEKEA siku ya uchangiaji damu duniani Juni 14 wananchi wametakiwa kuchangia damu hasa wenye makundi adimu ya damu.

Mwito huo umetolewa jana Jijini Dar es Salaam na Ofisa Uhamasishaji Mpango wa Damu Salama Kanda ya Mashariki, Evelyn Dielly wakati wa zoezi la uchangiaji damu lililo ratibiwa na Benki ya Equity.

Dielly alisema kuna na changamoto ya upatikanaji wa damu katika baadhi ya makundi ya damu ambayo ni adimu yakiwemo makundi ya O-, A-, B- na AB-.

“Anapopatikana mgonjwa wa O- halafu kukawa hakuna hamna katika Benki ya Damu kuna uwezekano mkubwa kumpoteza mgonjwa ni vyema wenye sifa za kuchangia damu na kundi lake ni O-,A-,B- au AB- akachangia damu ili benki iwe na damu ya kutosha”, alisema Dielly.

Alisema kuwa kuelekea siku ya uchangiaji damu dunia imepanga kukusanya chupa 1120 za damu salama “Wadau wakubwa wa uchangiaji ni wanafunzi wa shule za sekondari sasa wapo likizo kwahiyo tumehamia kwa wadau wengine leo tupo Equity kesho tutakiwa viwanja vya mnazimmoja, Mbezi kwa Magufuli na Mbagala” alisema.

Awali akizungumza katika uchangiaji damu Meneja Mwandamizi Rasilimali Watu Benki ya Equity, Fatma Msofe alisema kuwa wamehamasika kuchangia damu ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kukusanya damu salama na kuokoa maisha ya watu.

Alisema mahitaji ya damu ni makubwa hivyo ni jukumu la kila mmoja mwenye sifa za kuchangia akachangia “Hakuna kiwanda cha damu damu zinatoka kwetu sisi wenyewe, tafadhalini tujitokeze kwa wingi kuchangia damu ili tuokoe maisha” alisema Msofe.

Akizungumza baada ya kuchangia damu, Abdul Nasri alisema kuwa ameshawishika kuchangia damu kwa kuwa uhitaji wa damu salama katika jamii ni mkubwa.

Aidha Abdul aliwataka wenye sifa kuchangia damu kwa kuwa ni kitendo ambacho hakichukui muda mrefu na ni salama.

Kwa upande wake, Baraka Mumbila alisena kuwa amejitolea damu kwa ajili ya wenye uhitjai pia anaamini ipi siku na yeye atakuja kusaidiwa atakapohitaji.

“Hapa ukuchnagia damu wnakuweka katika orodha ya wanaochangia damu kwa hiyo siku ikitokea na wewe umepungukiwa unahitaji unapatiwa kwahiyo ni kama kujiwekea akiba mana sisi ni wanadamu hauwezi kujua ya kesho” alisema Baraka.

Kila ifikapo Juni 14 dunia inadhimisha siku ya uchangiaji damu duniani mwaka huu itaadhimisha miaka 20 ya uchangiaji damu.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents